TANGAZO


Friday, March 25, 2016

Kiongozi wa IS auwawa Syria

Abdul Rahman Mustafa al-Qaduli

Kiongozi wa pili kwa ukubwa katika itifaki ya kundi la wapiganaji la Islamic State ameuawa katika oparesheni iliotekelezwa na Marekani nchini Syria mwezi huu, vyombo vya habari vya Marekani vimesema.
Waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani Ash Carter alitarajiwa kuthibitisha kifo cha mwana jihad huyo na kutoa maelezo ya uvamizi huo.
Marekani ilikuwa imetoa zawadi ya dola milioni saba kwa mtu yeyote ambaye angetoa habari za Qaduli.
Qaduli alizaliwa mwaka 1957 ama 1959 kaskazini mwa mji wa Iraq wa Mosul ambao ulidhibitiwa na IS tangu mwaka 2014.
Alijiunga na al-Qaeda nchini Iraq mwaka 2004 chini ya uongozi wa marehemu Abu Musab al-Zarqawi akihudumu kama naibu wake na kiongozi wa eneo la Mosul kulingana na Marekani.
Baada ya kuachiliwa kutoka kwa jela za Iraq mapema mwaka 2012,alijiunga na vikosi vya IS nchini Syria.

No comments:

Post a Comment