TANGAZO


Wednesday, March 30, 2016

Wanaonyonyesha kwenda kazini na watoto Kenya

Image captionAkina mama wanaonyonyesha
Akina mama wenye watoto wachanga nchin Kenya wataweza kwenda kazini na wanao. Hii ni baada ya bunge kupitisha mswada wa Afya ambao utalazimu kampuni kutenga maeneo maalum ya kuwanyonyeshea watoto.
Maeneo hayo maalum yatakuwa na mashini ya kukamua maziwa ya mama, jokovu la kuhifadhi maziwa na chakula cha watoto pamoja na kuhakikisha mandhari sawa ya watoto wachanga.
Chini ya mswada huu waajiri lazima watoe muda kwa wanawake kuwanyonyesha watoto hao, kwa kupokezana.
Rachel Nyamai, mbunge aliyewasilisha mswada huo amesema utasaidia wanawake kufanya kazi vyema na wakati huohuo kuimarisha afya ya mtoto.
Image captionMtoto amelala
Kwa sasa ni mashirika machache sana nchini Kenya yanayotenga maeneo maalum ya wanawake kuwanyonyesha wanao.
Hii imewalazimu wanawake wengi kuwacha kuwanyonyesha watoto wao mapema kutokana na masharti na majira ya kazi.
Pendekezo sawa na hili lilitupwa nje na bunge lililopita baada ya tume ya waajiri kulalamika na kutishia kuwanyima kazi wanawake.
Image captionChumba maalum cha watoto
Mswada wa sasa wa Afya 2015 utawasilishwa kwa bunge ili kuidhinishwa kuwa sheria.

No comments:

Post a Comment