TANGAZO


Wednesday, March 23, 2016

UN: Watu 474 wameuawa Burundi

Rais Pierre Nkurunziza   
Ghasia za mauaji zilianza baada ya rais Pierre Nkurunziza pichani kutangaza nia yake ya kuwania muhula watatu
Takwimu mpya kutoka Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa watu 474 wamekwishauawa nchini Burundi tangu mwezi Aprili mwaka jana, wakati mzozo ulipoibuka kufuatia uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu madarakani.
silaha 
Serikali ya Burundi inasema mauaji yalitekelezwa na waasi
Lakini kiongozi wa shirika la haki za binadamu la Burundi amesema kuwa idadi ya waliouawa inazidi watu 600.
Muakilishi wa serikali ya Burundia amesema kuwa mauji yalitekelezwa na waasi.
mtaani Bujumbura 
Mauji dhidi ya viongozi wa kijeshi yamekua yakitekelezwa kwenye maeneo ya mji wa Bujumbura
Jumanne, afisa wa ngazi ya juu wa kijeshi na mshirika wa rais alipigwa risasi na kuuawa kwenye ofisi ya wizara ya ulinzi.
Meja mwingine ameripotiwa kupigwa risasi na kuuawa usiku wa kuamkia leo alipokua akiondoka kwenye baa katikati mwa mji mkuu, Bujumbura.

No comments:

Post a Comment