Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesema kwamba mataifa yote ya bara Ulaya yanafaa kuweka kando kile anachokiita mchezo wa kisiasa wa kijiografia na kuanzisha ushirikiano.
Bwana Lavrov ameomba kuwepo kwa ushirikiano na umoja dhidi ya vitisho vya kigaidi-- huku akisema kwamba magaidi hawafai kuachiwa nafasi ya kujigamba na kufanya watakalo katika bara Ulaya.Lavrov amesema hayo kabla ya kuanza mazungumzo na mwenzake wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier.
Naye Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls ameyashutumu mataifa ya bara Ulaya kwa "kufumbia macho" vitisho vya makundi yenye itikadi kali ya kiislamu.
Bwana Valls, ameiambia radio moja ya Ufaransa kuwa, pana haja ya kuongeza ulinzi mkali katika mipaka ya mataifa ya Jumuia ya bara Ulaya ili kuzuia mashambulizi kama ya jana yaliyotokea Brussels-Ubelgiji.
No comments:
Post a Comment