TANGAZO


Wednesday, March 30, 2016

Mtekaji nyara awekwa rumande Cyprus

Image copyrightEPA
Image captionMtekaji nyara awekwa rumande Cyprus
Mwanaume aliyejisalimisha kwa polisi wa Cyprus baada ya kuteka nyara ndege ya Egypt Air amefikishwa mahakamani.
Seif Eldin Mustafa amewekwa rumande kwa siku 8 ilikuruhusu uchunguzi ukamilishwe.
Mahakama hiyo ya Larnaca inapanga kumfungulia mshukiwa huyo mashtaka ya utekaji nyara, na kutishia maisha ya abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya Egypt Air.
Hakuruhusiwa kuzungumza ila alionesha alama ya ushindi alipokuwa akiondolewa mahakamani.
Maafisa wakuu wa Cyprus wanasema kuwa wanaona dalili kuwa Mustafa anamatatizo ya kiakili wakisema tukio hilo la utekaji nyara halihusiani kwa njia yeyote na ugaidi.
Image captionHakuruhusiwa kuzungumza ila alionesha alama ya ushindi alipokuwa akiondolewa mahakamani.
Ndege hiyo ya EgyptAir MS181 ilikuwa ikibeba abiria 55, ikiwemo raia 26 wa kigeni waliotoka Alexandria kueleka Cairo.
Wengi wa wale waliokuwa wameabiri ndege hiyo waliwachiliwa baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa ndege wa Lanarca lakini mtekaji huyo aliwazuia watu saba kabla ya kisa hicho kukamilika kwa amani.
Waziri wa maswala ya nje wa Cyprus Ioannis Kasoulides alisema kuwa bw Mustafa aliomba kuzungumza na mkewe wa zamani ambaye aliletwa katika uwanja wa ndege na polisi kabla ya kuanza kutoa matakwa mengine ya ''yasiyo na maana''.

No comments:

Post a Comment