TANGAZO


Thursday, March 17, 2016

Miss Tanzania kuzinduliwa keshokutwa Jumamosi Machi 19, 2016

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akitangaza siku ya uzinduzi wa mashindano hayo, utakaofanyika Jumamosi Machi 19, mwaka huu jijini. Katikati ni Miss Tanzania 2014-2015, Lilian Kamazima. (Picha zote na Kassi Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akitangaza siku ya uzinduzi wa mashindano hayo, utakaofanyika Jumamosi Machi 19, mwaka huu jijini. Kulia ni mmoja wa waratibu wa shindano hilo, Bosco Majaliwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uzinduzi huo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu uzinduzi wa shindano hilo, Dar es Salaam leo.

Baadhi ya waandishi wa habari, wakichukua habari zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, kuhusu uzinduzi wa shindano hilo, Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga,
Baadhi ya wapigapicha za habari, wakichukua habari zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, kuhusu uzinduzi wa shindano hilo, Dar es Salaam leo.


MSIMU mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 utazinduliwa rasmi siku ya Jumamosi tarehe 19 Machi 2016 katika Hotel ya Ramada Resort iliyopo eneo la Kunduchi jijini D’salaam.

Katika uzinduzi huu utawakutanisha wadau mbalimbali wa tasnia ya urembo wakiwemo Wabunifu wa mavazi, mawakala wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi mbalimbali hapa nchini.

Wengine ni Wakurugenzi wa Makampuni mbalimbali amboa miongoni mwao wanatarajia kuwa wadhamini wa shindano hili kwa mwaka huu 2016.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo Mheshimiwa Nape Moses Nnauye.

Burudani kadhaa zitanogesha uzinduzi huo akiwemo msanii wa kizazi kipya aitwae Linah Sanga pamoja na Msanii wa ngoma za asili Wanne Star.

Uzinduzi wa Miss Tanzania kwa mwaka 2016 utakuwa wa aina yake kwani mara tu baada ya uzinduzi huu katika jiji la D’slaam, utahamia mkoa wa Arusha ambako pia kutakuwa na aina nyingine ya uzinduzi.

Mara baada ya uzinduzi huo Ratiba ya semina ya mawakala itaafuatia hapo baadae na kuanza kwa mashindano ya urembo katika ngzi za vituo, wilaya, Mikoa na Kanda.

Hadi sasa wadhamini kadhaa wamejitokeza na kuonyesha nia ya kutaka kudhamini shindano ili katika ngazi Taifa.

Uzinduzi wa shindano la Urembo la Miss Tanzania 2016 umedhaminiwa na Makampuni yafuatayo

Ramada Resorts Dar
Naf Beach hotel Mtwara
Kitwe General Trader
CXC Africa
MMI Tanzania
Mwandago Investment Ltd.
BreakPoint                                                                                                                                                                                                                                                    
GSM Media
Inatolewa na

HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI
LINO INTERNATIONAL AGENCY LTD

No comments:

Post a Comment