Na Beatrice
Lyimo-MAELEZO
21/03/2016
Dar es Salaam.
UONGOZI wa Kampuni ya
Kikundi cha Waathirika wa Maendeleo (Kichawa) unaojishughulisha na usafirishaji
wa mizigo wamezindua mwongozo wa mfumo shirikishi
wa uratibu wa Bodaboda na Bajaji nchini.
Akizindua mfumo huo
leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Mussa Chengulla na
kusema kuwa lengo ni kupambana na kupata suluhiso la kudumu katika sekta ya
usafirishaji wa Bodaboda na Bajaji juu ya changamoto za kisheria, kiusalama na
kimazingira.
Chengulla amesema
kuwa sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa mfumo huo ni matokeo makubwa ya
changamoto zilizojitokeza katika jamii juu ya wizi wa pikipiki, wizi wa kutumia
pikipiki, uvunjifu wa sheria za usalama barabarani, kanuni za usafirishaji,
matumizi ya kujichukulia sheria mkononi, uegeshaji holela wa bodaboda na bajaji
na ukamataji usio salama.
“Uwanzishwaji wa mfumo huu shirikishi ni
kukabiliana na changamoto zitokanazo katika sekta ya usafirishaji na kutatua kero hatarishi zinazoikabili
jamii ili kufika malengo ya kuiondoa ajira ya bodaboda na bajaji katika orodha
ya ajira hatarishi, kero na janga la Taifa na kuifanya kuwa ajira tegemezi,
endelevu na salama kwa usalama wa raia na mali zao” aliongeza Bw. Chengulla.
Mbali na hayo Bw.
Chengulla amesema kuwa watakaonufaika na mfumo shirikishi ni TAMISEMI Halmashauri
ya Manispaa ya Wilaya kwa kutambua idadi kamili ya wanaoendelea kujiajiri na
kuajiriwa kupitia sekta ya usafirishaji abiria.
Pia wengine
watakaonufaika na mfumo huo shirikishi ni SUMATRA, Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA),
Jeshi la Polisi na Usalama ya Raia na kitengo cha usalama barabarani, wamiliki
na madereva wa bodaboda na bajaji kulingana na kazi za sekta husika.
No comments:
Post a Comment