TANGAZO


Monday, March 28, 2016

Fidel Castro akosoa ziara ya Obama Cuba

Castro

Image copyrightGetty
Image captionFidel Castro amesema ahadi za Obama zinaweza kuwapa raia wa Cuba "mshtuko wa moyo"
Aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa Cuba Fidel Castro amevunja kimya chake kuhusu ziara ya hivi majuzi ya Rais wa Marekani Barack Obama nchini humo.
Kwenye barua iliyochapishwa katika gazeti la serikali ya nchi hiyo la Granma kiongozi huyo ameonekana kukosoa ziara hiyo.
Fidel, aliyemkabidhi kakake Raul uongozi wa taifa hilo mwongo mmoja uliopita, amesema Cuba haihitaji zawadi zozote kutoka kwa Marekani.
ZiaraImage copyrightAFP
Image captionKwenye ziara hiyo, Bw Obama alijibizana na Raul Castro
Akijibu pendekezo la Bw Obama kwamba wakati umefika wa kuunda urafiki na kuzika kwenye kaburi la sahau masalio ya Vita Baridi bara Amerika, Fidel Castro amewakumbusha wasomaji kuhusu uvamizi wa Bay of Pigs uliofanywa na wakimbizi wa Cuba wakisaidiwa na Marekani mwaka 1961.
Amesema maneno ya Obama ya kuhimiza maridhiano ni sawa na “rojo ya sukari” na kuonya kwamba raia wa Cuba wanaweza kupata “mshtuko wa moyo”.
Fidel Castro, 89, aliongoza Cuba kuanzia 1959 hadi 2008 alipomkabidhi nduguye madaraka.

No comments:

Post a Comment