Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja
miradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Eng. John Msemo wakati alipotembelea
daraja la Kigamboni kuangalia ujenzi wa daraja la Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.
Mwonekano wa lango la
kuingilia daraja la Kigamboni kwa upande
wa Kigamboni, linavyoonekana pamoja na vyumba vya kukatia tiketi.
Mwonekano wa vyumba
vya ofisi zitakazotumiwa na wasimamizi wa Daraja la Kigamboni.
Mwonekano wa daraja la
Kigamboni ambalo litafunguliwa rasmi mwezi ujao.
Barabara za maingilio
(inter change) ya Daraja la Kigamboni upande wa Kurasini.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipata maelezo kutoka kwa
Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni Eng. Karim Mattaka alipokagua
daraja hilo leo jijini Dar es Salaam. (Zimetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)
WAZIRI wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema daraja la Kigamboni
litafunguliwa rasmi Aprili, 16 mwaka huu.
Amesema kazi inayoendelea
sasa hivi ni kupitisha magari maalum kwa ajili ya kupima ubora wa daraja hilo
ili kujiridhisha kabla ya kukabidhiwa rasmi Serikalini.
Amewataka watumiaji wa
daraja hilo kuwa waangalifu, kulinda miundombinu na kuepuka vitendo vya hujuma ili lidumu kwa muda mrefu.
“Daraja hili lina
urefu wa mita 640, barabara sita, tatu zinapanda na tatu zinashuka, hivyo
tunawaomba wananchi watakaovuka kuzingatia usafi na ustaarabu”, amesema Profesa
Mbarawa.
Amebainisha kuwa
Serikali itaweka sheria kali kwa wote watakaokiuka matumizi sahihi ya daraja
hilo na kusisitiza umuhimu wa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani
wanapovuka katika daraja hilo.
Meneja Msimamizi wa
ujenzi wa daraja hilo Eng. Karim Mattaka amesema wataalam wanaendelea na
taratibu za kulipima daraja hilo ili kujiridhisha kama linamudu kupitisha uzito
uliokusudiwa kabla ya kulikabidhi kwa Serikali mapema mwezi ujao.
Amesema awamu ya
kwanza ya kulipima daraja hilo imekamilika na sasa wanaendelea na awamu ya pili
hadi watakapomaliza awamu nne ili kujiridhisha kabla ya kuanza kutumika.
Takribani shilingi
bilioni 216 zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo linalotazamiwa kupunguza
kwa kiasi kikubwa msongamano wa abiria na magari katika kivuko cha Magogoni na
Kigamboni.

No comments:
Post a Comment