TANGAZO


Friday, March 18, 2016

Ajuza aliyemualika Obama apata majibu Cuba

   
Mwanamke wa Cuba
Mwanamke mmoja aliyemwalika rais wa Marekani Barrack Obama nyumbani kwake nchini Cuba amepokea majibu kutoka kwa rais huyo baada ya mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Marekani na Cuba kurejeshwa.
Barua hiyo inayompatia asante bi Yarza ilipelekwa nchini Cuba siku ya Jumatano.
 
Barua ya Obama
Zilikuwa barua za kwanza kuwasili nchini Cuba kutoka Marekani baada ya kipindi cha miaka 50.
Mawasiliano ya kutuma ujumbe wa moja kwa moja kati ya mataifa hayo mawili yalikatizwa wakati wa vita baridi,huku barua zilizoandikwa zikipitia mataifa mengine kama vile Mexico na Canada.
Bi Yarza aliandika kwa Obama mnamo tarehe 18 mwezi Februari baada ya kugundua kwamba anajiandaa kuizuru Cuba mnamo mwezi Machi,akimwabia:Raia wa Cuba ambao wangependelea kukutana nawe kibinafsi ni wachache.
Barua ilioandikwa na Obama
Rais Obama alimshukuru Bi Yarza kwa usaidizi wake akiongezea kuwa barua hiyo ni ishara ya uhusiano mzuri katika siku za usoni kati ya mataifa hayo mawili.
Na hakumpuuza kuhusu kikombe cha chai akisema kuwa atatafuta muda.

No comments:

Post a Comment