TANGAZO


Friday, January 15, 2016

Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kuendelea kushirikiana na wajasiriamali wa kazi za Sanaa Peo

Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiriamali wa kazi za Sanaa Bw. Henry  Clemens akiishukuru Serikali kwa kuonyesha nia ya kuwasaidia kwa kuanzisha Idara ya Sanaa na hivyo wataitumia kuimarisha kazi zao ili ziwanufaishe. Pembeni yake ni Makamu Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Bw. Chief Eliewaha Shogholo Challi. 
Baadhi ya wajasiriamali wa kazi za Sanaa wa Mikono Cultural Heritage Ltd wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bi Leah Kihimbi (hayupopichani) leo jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiriamali wa kazi za Sanaa Bw. Henry Clemens (kushoto) akimweleza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi Leah Kihimbi (kulia). Bw. Clemens aliomba Serikali kuwawezesha kupata wawekezaji, na pia shughuli za Sanaa ziwe rasmi ili wajipatie kipato na kutengeneza ajira kwani wazalishaji wa Sanaa wanafikia milioni 3 kwa sasa. 
Kaimu Mkurugenzi Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi akiongea na wajasiriamali wa kaziza Sanaa wa Mikono Cultural Heritage Ltd walipo mtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Bi. Leah aliwahaidi wasanii hao kufanya nao kazi kwa karibu na kuwapa ushirikiano mkubwa katika kazi zao. 
Wakiwa katika picha ya pamoja. (Picha zote na Daudi Manongi-WHUSM)

No comments:

Post a Comment