TANGAZO


Friday, January 15, 2016

Matokeo mtihani kidao cha pili 2015 yatangazwa

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk. Charles Msonde.

Mwandishi wetu
BARAZA la Mitihani Tanzania (Necta), limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha pili (FTNA) ambapo liliweka wazi kuwa somo la Hisabati lina ufaulu wa chini zaidi katika masomo yote.

Aidha wanafunzi 39,567 sawa na asilimia 10.88 wanatarajia kurudia mtihani kutokana kushindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu mwaka huu.

Akitangaza matokeo hayo  Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Charles Msonde alisema kuwa wanafunzi 396,770 waliandikishwa kufanya upimaji wa Kitaifa, wakiwemo wasichana 199,615 sawa na asilimia 50.31 na wavulana 197,155 sawa na asilimia 49.69.

Alisema kati yao wanafunzi 396,770 waliosajiliwa, 363,666 sawa na asilimia 91.66 walifanya upimaji wa kitaifa ambapo wasichana walikuwa ni 184,895 sawa na asilimia 92.63 na wavulana ni 178,771 sawa na asilimia 90.68.

Aidha alisema wanafunzi 33,104 sawa na asilimia 8.34 hawakufanya upimaji huo kwa sababu za utoro na ugonjwa.

Dk. Msonde alisema upimaji huo unaonesha kuwa jumla ya wanafunzi 324,068 sawa na asilimia 89.12 wamepata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu mwaka huu.

Alisema kati yao wasichana ni 164,547 sawa na asilimia 89.00 na wavulana ni 159,521 sawa na asilimia 89.24 huku 39,567 sawa ana silimia 10.88 wakirudia mtihani kutokana na kukosa alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.

Aidha alisema kwa mwaka 2014 wanafunzi 375,434 sawa ana silimia 92.66 walipata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

Akizungumzia ubora wa ufaulu alisema idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya Distinction, Merit na Credit ni 155,667 sawa na asilimia 42.80 wakiwemo wasichana 68,780 sawa na asilimia 37.20 na wavulana 86,887 sawa na asilimia 48.60.

Kwa upande wa ufaulu wa masomo alisema katika masomo ya msingi ya Kiswahili, Commerce na Kemia umepanda kidogo ikilinganishwa na mwaka 2014. Aidha ufaulu kwa masomo ya uraia, Historia, jiografia, kingereza, fizikia, biolojia, hisabati na Book Keeping umeshuka kidogo kidogo ikilinganishwa na mwaka 2014.

Somo lililofanyika vizuri zaidi katika FTNA mwaka jana ni kiswahili ambapo asilimia 86.34 ya wanafunzi wamefaulu na somo lenye ufaulu wa chini zaidi ni Hisabati ambalo ufaulu wake ni asilimia 15.21.

Shule 10 bora
Mwanza Alliances(Mwanza), Alliance Girls (Mwanza), Alliance Rock Army (Mwanza), St. Francis Girls (Mbeya), Bethel Sabs Girls Mafinga (Iringa), Shamsiye Boys, Feza Boys, Feza Girls, Canossa (zote Dar es Salaam) na Don Bosco Seminary (Iringa)

Shule 10 bora za mwisho

Michenjele (Mtwara), Furaha (Dar es Salaam), Mdando, Mlongwema, Kwai(Zote za Tanga), Lionja(Lindi), Mkoreha(Mtwara),Mlungui(Tanga), Makong'onda(Mtwara)na Kwaluguru(Tanga). 

Watahiniwa 10 bora kitaifa

Lineth Christopher (ST.Aloysius Girls)Pwani, Jerry Panga(Marian Boys)Pwani, Rhobi Simba(Marian Girls) Pwani, Colin Emmanuel(Feza Boys)Dar es Salaam, Nickson Maro(Magnificat)Kilimanjaro, Diana Mwakibinga (Morning Star)Mwanza, Elisha Peter(Buswelu)Mwanza, Gaudencia Lwitakubi(Allience Girls)Mwanza, Fuad Thabit(Feza Boys), Dar es Salaam na Geraldina Kyanyaka(Canossa)Dar es Salaam.

Wasichana 10 bora kitaifa
Lineth Christopher (ST.Aloysius Girls) Pwani, Rhobi Simba (Marian Girls) Pwani, Diana Mwakibinga (Morning Star) Mwanza, Gaudencia Lwitakubi (Allience Girls) Mwanza, Geraldina Kyanyaka (Canossa) Dar es Salaam, Ranata Chikola (St.Aloysius Girls) Pwani, Happiness Mwailunga (Canossa) Dar es Salaam, Monica Tesha (St.Aloysius Girls) Pwani, Judith Amos (Precious Blood) Arusha na Amina Khalfan (Feza Girls) Dar es Salaam.

Wavulana 10 bora kitaifa

Jerry Panga (Marian boys) Pwani, Colin Emmanuel (Feza Boys)Dar es Salaam, Nickson Maro (Magnificat) Kilimanjaro, Elisha Peter(Buswelu)Mwanza, Fuad Thabit(Feza Boys) Dar es Salaam, Mwinangwa Chibunde (Mwanza Alliance) Mwanza, Baraka Muhammed (Eagles) Pwani, Joshua Kafula (Libermann Boys), Dar es Salaam, Emmanuel Magombi
(Moring Star) na Frank Charles(Marist Boys) Mwanza. 

Dk. Msonde alisema jitihada za makusudi zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa baadhi ya masomo ambayo hayakufanyika vizuri.

Hata Baraza hili liliwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri na kupata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya sekondani ya kidato cha tatu kwa mwaka huu na kuwatakia kuendeleza bidii katika kujifunza ili kuimarika zaidi kitaaluma kabla ya kuingia kidato cha nne.

"Baraza linatoa mwito kwa walimu na wanafunzi kuendeleza juhudi katika ufundishaji na ujifunzaji katika amsomo yaliyofanyika vizuri ili waweze kuendelea kuimarika zaidi katika masomo hayo watakapokuwa kidato cha tatu,"alisema.

Kwa upande wa wazazi, walezi na wadau mbalimbali wa elimu aliwataka kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa walimu na viongozi wa elimu katika kluboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji masjhuleni ili kuwezesha wanafunzi kupata elimu inayotarajiwa. 

No comments:

Post a Comment