TANGAZO


Wednesday, December 16, 2015

Wawindaji kutoka Qatar watekwa nyara Iraq

Iraq

Image copyrightAFP
Image captionIraq ni moja ya mataifa yanayopendwa sana na wawindaji wa Uarabuni
Watu wenye silaha wamewateka nyara wawindani 27 kutoka Qatar, miongoni mwao watu wa familia ya kifalme, polisi na gavana wa eneo wamesema.
Wawindaji hao wametekwa katika eneo la jangwani nchini Iraq karibu na mpaka wa taifa hilo na Saudi Arabia.
Washambuliaji waliokuwa na magari kadha walishambulia kambi ya wawindaji hao mapema asubuhi.
Kambi hiyo ilikuwa eneo la Layyah, kilomita 190 kutoka mji wa Samawa.
Operesheni kubwa ya kuwasaka imeanzishwa.
Kufikia sasa, hakuna tamko lolote kutoka kwa maafisa wa serikali ya Qatar.
Eneo ambako kisa kilitokea linadhibitiwa na makundi ya kikabila na wakazi ni wa dhehebu la Shia, mwandishi wa BBC aliyeko Beirut Jim Muir anasema.
Vyama vya kisiasa vya Kishia vinavyodhibiti serikali ya Iraq vimekuwa vikikosoa sana Qatar kwa kuunga mkono wapiganaji wa Kisunni nchini Syria.
Hii ina maana kwamba huenda kisa hiki kikasababisha mzozo wa kidiplomasia, mwandishi huyo anasema.
Afisa wa polisi kutoka Samawa, mji mkuu wa eneo la Muthanna, amesema washambuliaji huenda walifika 100.

No comments:

Post a Comment