Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akimkaribisha ofisini kwake
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Times Tanzania Bi. Zuhura Hanif leo jijini
Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akielezea jambo wakati wa mazungumzo baina yake na uongozi wa Star Times waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang na Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue. Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xueafafanua jambo wakati wa mazungumzo baina ya wawakilishi wa StarTimes na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofangakielezea jambo wakati wa mazungumzo baina ya wawakilishi wa StarTimes na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya Kadi ya Krismasi aliyokabidhiwa kwa niaba ya uongozi wa StarTimes Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang. Katikati ni Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akishukuru mara baada ya kupokea zawadi ya Kadi ya Krismasi aliyokabidhiwa kwa niaba ya uongozi wa StarTimes Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang (kushoto). Katikati ni Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (mwenye tai), akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa StarTimes kwa kumtembelea ofisini kwake na kuipongeza Serikali kwa ushirikiano inaowapa katika kutekeleza wajibu wao kama wabia wa habari hapa nchini. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Bw. Assah Mwambene, Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang, Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania Bi. Zuhura Hanif.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (katikati), akiwa katika picha ya
pamoja na wawakilishi wa StarTimes Tanzania walipomtembelea ofisini kwake leo
jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO
Bw. Assah Mwambene, Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue, Ofisa Mtendaji
Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang na Makamu wa Rais wa StarTimes
Tanzania Bi. Zuhura Hanif. (Picha zote na Frank Shija, Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini WHUSM)









No comments:
Post a Comment