Waziri Angella Kairuki.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya
Rais - Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) ameelekeza ni lazima
kufanya kazi kwa ushirikiano Serikalini ili kufikia lengo.
Waziri Kairuki alisema hayo jana
katika kikao kazi na Wafanyakazi wa Idara ya Mipango-UTUMISHI.
“ Kufanya kazi kwa ushirikiano
ni muhimu ili tufikie malengo tuliyoweka katika Utumishi wa Umma” Mhe. Kairuki
alisema na kusisitiza ni jambo lisilopingika kuwa muda mwingi hutumika na Watumishi
katika kazi hivyo utamaduni na nidhamu ya kushirikiana ni muhimu ili kuongeza
kasi ya kazi na matokeo yasiyokuwa ya kubahatisha.
Mhe. Kairuki alitoa fursa
kwa Watumishi wa Umma wenye maoni kuhusu utendaji kazi Serikalini wasikae nayo
bali wafike ofisini kwake na kushauri ili wananchi wapate huduma bora zaidi na
zenye kiwango kutoka kwa Serikali yao.
Waziri Kairuki alisisitiza
kushirikiana kwa karibu na Watumishi nchini ili kuleta maendeleo na kuondokana
na mtazamo wa kupokea yanayosemwa na viongozi bila kushauri au kuboresha zaidi.
Mhe. Kairuki ameanzisha
utamaduni wa kazi kwa kukutana na Watumishi wa Umma ili kubaini changamoto na
kuzifanyia kazi. Wiki hii ameanza na Idara na Vitengo vya ofisi yake.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi
ya Rais-Utumishi na Utawala Bora.


No comments:
Post a Comment