Meneja wa Operesheni wa Kampuni ya CMEA
(Copyright Mnagement East Africa), ambao imetengeneza utaratibu wa kusimamia hakimiliki za kazi za wasanii wa ukanda wa Afrika Mashariki akichangia jambo katika mkutano na waandishi wa habari juu ya wasanii kuanza kulipwa mirahaba kuanzia mwakani na wamiliki wa vyombo vya habari.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo (kushoto), akiwa pamoja na Ofisa Mtendaji wa
COSOTA Bi. Doreen Sinare (katikati) na Paul Matthysse ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMEA wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya vyombo vya habari kuanza kulipia mirahaba kwa wasanii wa muziki kuanzia mwakani.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiongea na wadau mbalimbali kutoka
BASATA, COSOTA, BODI YA FILAMU, CMEA NA WASANII leo hii jijini Dar es Salaam, juu ya kuendelea kusimamia haki ya wasanii na kuhakikisha kila msanii anapata anachostahili kupitia sanaa yake na kwamba Serikali imeweka nguvu kubwa katika eneo hilo.
Mwanamuziki wa kundi
la Weusi Bw. Nikki wa Pili akichangia hoja katika mkutano na waandishi wa habari juu ya wao kuanza kulipwa mirahaba kupitia kazi zao. Nikki wa Pili aliiomba Serikali kupunguza kodi katika vifaa vya kurekodia filamu na muziki ili wasanii watoe kazi nzuri zaidi na pia Sera ielekezwe katika kuboresha teknolojia ili wasanii wafaidike.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (kulia), akiongea waandishi wa habari kuhusu vyombo vya habari (television na Redio)
kuanza kulipia mirahaba kwa wasanii wa muziki leo hii jijini Dar es Salaam. Mhe. Mwijage aliwasisistiza wasanii kwenda
COSOTA kuandikisha kazi zao ili zitambulike na wafaidike kwa kulipwa mirahaba.

No comments:
Post a Comment