TANGAZO


Thursday, December 10, 2015

Olunga wa Gor Mahia ashinda tuzo kuu Kenya

Olunga


Image captionOlunga alisaidia Gor Mahia kutwaa ubingwa wa ligi Kenya

Mshambuliaji wa Gor Mahia Michael Olunga ametawazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora zaidi wa mwaka 2015 nchini Kenya.
Mshambuliaji huyo wa timu ya Gor Mahia ametuzwa kombe hilo pamoja na kitita cha shilingi milioni moja za Kenya au dola elfu kumi mbali na zawadi nyinginezo kama vile TV kubwa ya inchi 43.


Mwanahabari wa BBC Shaaban Ndege anasema sherehe za mwaka huu za kuwatuza wachezaji bora wa kandanda nchini Kenya zilikuwa za kipekee kwani mbali na miaka ya nyuma, kitita kikubwa cha pesa kilitumika kuwapa washindi wa karibu kila kitengo.
Kulikuwa na jumla ya vitengo 13 vya kushindaniwa, huku walioibuka washindi wakipewa pesa taslimu au zawadi chungu nzima zilizotolewa na kampuni mbalimbali za wafadhili.
Licha ya mwenyekiti wa soka Nchini Kenya Sam Nyamweya na waziri wa michezo Hassan Wario wakikwepa kuhudhuria sherehe hizo, zilizofanyika katika hoteli moja ya kifahari Jijini Nairobi, nyota wa zamani wa soka nchini Kenya walihudhuria akiwemo J.J Masiga.
Tuzo ya mwaka huu ya mchezaji bora wa mwaka lilimwendea chipukizi wa miaka 22 mwanafunzi wa chuo cha teknolojia cha Kenya na mshambulizi wa Gor Mahia Michael Olunga.
Tuzo mpya iliyobuniwa mwaka huu ya mchezaji chipukizi zaidi wa mwaka, ilimuendea George Mandela wa timu ya Muhoroni FC, kutoka Magharibi mwa Kenya.
Nayo tuzo ya refa aliyeimarika zaidi mwaka huu, ilitwaliwa na Raymond Onyango na ile ya naibu kocha ikatwaliwa na Stephen Deya.
Nayo timu bora zaidi mwaka 2015 ilikuwa Western Stima baada ya kuzipiku Mathare United na Sony Sugar.
John Baraza wa timu ya Sofapaka alinyakuwa tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu ya hali ya juu zaidi mwaka huu.
Ushindani mkali ulishuhudiwa katika tuzo la maneja bora zaidi wa timu, ambapo hatimaye Bw Jodali Obondo wa Gor Mahia aliibuka mshindi.
Katika wachezaji, kipa bora mwaka huu wa KPL alikuwa Bonface Oluoch wa Gor Mahia aliyejipatia dola elfu tano, huku Farouk Shikalo wa Muhoroni Youth na Jairus Adira wa wakijipatia dola elfu mbili kila mmoja.
Mlinzi bora alikuwa mchezaji wa Gor Mahia raia wa Burundi, Karim Nzigimana.
Tuzo la Kocha bora lilimweendea mkufunzi wa mabingwa wa ligi kuu nchini Kenya Gor Mahia, Frank Nutall, ambaye alipewa mkataba huo kwa misingi kuwa sharti aifanye timu ya Gor kuibuka mshindi ili apate kazi ya ukufunzi, jambo ambalo amelitimiza.

No comments:

Post a Comment