Mahakama kuu nchini Japan imedumisha sheria kwamba watu waliooana ni lazima watumie jina moja la kiukoo.
Hatua ni pigo kubwa kwa wanaharakati wa kutetea haki za wanawake ambao walitaka wanawake waruhusiwe kutumia majina ya kiukoo ya wazazi wao, sawa na walivyofanya kabla ya karne ya 19.
Wanaharakati wamesema kuwa sheria hiyo ina ubaguzi kwani wanandoa wengi hulazimika kutumia jina la kiukoo la waume zao.
Lakini mahakama imesema kwamba sheria hiyo haiendi kinyume na katiba ya nchi.
Mahakama hiyo hata hivyo imebatilisha sheria iliyowazuia wanawake kuolewa kabla ya miezi sita kupita baada yao kupewa talaka.
Sheria zote mbili zilianza kutekelezwa enzi ya Meiji katika karne ya 19.
Jaji Itsuro Terada amesema kuwa miongoni mwa Wajapani tayari kunayo matumizi yasiyo rasmi ya kuendelea kutumia jina la kifamilia la mwanamke, jambo ambalo linakosesha nguvu kiasi sheria ya majina ya kifamilia.
Amesema kuwa wabunge wanafaa kuamua iwapo watapitisha sheria mpya kuhusu majina ya kifamilia au la.
Gazeti la The Japan Times, limeangazia utafiti uliofanyika katika kipindi cha miaka 40 iliyopita ambao unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 96 ya wanawake waliolewa nchini Japan wanapendelea kutumia jina la familia la waume zao.
No comments:
Post a Comment