TANGAZO


Wednesday, December 16, 2015

Magufuli amfuta mkuu wa kupambana na rushwa

Magufuli

Image copyrightStatehouse Tanzania
Image captionMagufuli amesema hajaridhishwa na utendakazi wa mkuu huyo
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dkt Edward Hoseah, na pia akawasimamisha kazi maafisa wa nne wa taasisi hiyo.
Rais Magufuli amesema hajaridhishwa "na namna taasisi hiyo ilivyokua ikitekeleza wajibu wake katika kukabiliana na rushwa hususani kwenye upotevu wa mapato ya serikali katika bandari ya Dar es salaam.”
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Dkt Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Bw Valentino Mlowola kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.
Kwa mujibu wa Bw Sefue, Dkt Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa "utendaji kazi wa Takururu chini ya Dkt Edward Hoseah hauwezi kuendana na kazi anayoitaka”.
Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Takururu ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.
Bw Sefue amesema atakayekiuka agizo la rais "atachukuliwa hatua kali”.
Hii si mara ya kwanza kwa Dkt Magufuli kuwachukulia hatua maafisa wa Serikali tangu achukue madaraka mwezi uliopita. Siku chache baada ya kuingia afisini, alibadilisha usimamizi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kufanya ziara ya kushtukiza huko na kutoridhishwa na utoaji huduma.
Majuzi alivunja bodi inayosimamia bandari.

No comments:

Post a Comment