Na Tupokigwe Marco na Mwanahamisi Matasi.
CHAMA cha Sanaa cha uchoraji picha maarufu kama Tinga Tinga kimetiliana saini Mkataba wa Makubaliano wa miaka mitano wa kufanya kazi kwa pamoja na Kampuni ya
Bricoleur Holdings Co. Ltd ya nchini Japan utakaokiwezesha chama hicho
kunufaika kwa kuuza kazi zake Kimataifa.
Akiongea leo
wakati wa utiaji saini wa Mkataba huo, Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa cha
Tinga Tinga, Bwana Zachi Chimwanda ameeleza kuwa, utiaji saini wa Mkataba huo
utakua chachu ya maendeleo katika kuwakomboa wasanii wachoraji katika kipato
chao na kuboresha hali zao za kimaisha kwakuwa kazi zao sasa zitakuwa zikiuzwa
ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake
Katibu Mtendaji wa Baraza la Wasanii la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza
alieleza kuwa Mkataba waliosaini kati ya Tinga Tinga na watu wa Bricoleur
Holdings Co. Ltd utaimarisha kazi za Wasanii katika fani ya uchoraji ikiwemo
kuongeza vipato vyao.
''Sanaa ni kazi
lakini pia ni biashara, imefika wakati kwa wasanii kufaidika na jasho lao,
kampuni hii watakua wakitafuta masoko kule Japan ili kazi hizi za wachoraji
toka Tanzania ziweze kununuliwa hali ambayo itawaongezea kipato'', alisema
Mngereza.
Aliongeza kuwa
Mkataba uliosainiwa kati ya pande zote mbili umepitia taratibu zote za
kiserikali na Taasisi zinazohusika na mambo ya sanaa na maslahi ya msanii na
msanii yule aliyehusika katika kuchora picha fulani atanufaika na mkataba huo.
''Kwa msanii
atakehusika binafsi na uchoraji picha mkataba utamwezesha kujua atanufaika vipi
na kwa muda gani'', aliongeza Mngereza.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings Co. Ltd, Bi. Yu Shiran ameeleza
kuwa mpango huo wa Mkataba kati yao na Tingatinga una lengo la kukitangaza
Chama hicho cha wachoraji wa Tanzania Kimataifa.
‘’Kwa kutumia taarifa
za kidijiti za Tingatinga tutaweza kushirikiana na watengenezaji mbalimbali wa
bidhaa, na ili kulithibitisha hili, sisi na Tingatinga tumekuwa katika mjadala wa
takriban mwaka mzima sasa’’, alisema Bi. Shiran.
Tingatinga Arts
Group lilianzishwa nchini Tanzanja na Edward Saidi Tingatinga ambaye alifariki
mwaka 1972 ambapo kwa sasa kundi hilo lipo maeneo ya Oysterbay jijini Dar es
Salaam kikijihusisha na sanaa ya uchoraji.
No comments:
Post a Comment