TANGAZO


Saturday, November 21, 2015

Watu 7 wafariki katika ajali ya ndege N Zealand

Image captionNdege ilioanguka katika barafu huko New Zealand
Polisi wa New Zealand wanasema kuwa watu wote saba walioabiri ndege iloanguka katika kisiwa cha South Island wamefariki.
Helikopta waliyokuwa ndani ilianguka katika eneo la Fox Glacier, eneo lililo mbali ingawa ni maarufu sana kwa watalii katika ufuo wa Magharibi.
Helikopta nne zimetumwa eneo hilo kwa uwokozi na kutafuta mabaki ya ndege.
Image captionBarafu nchini New Zealand
Shughuli hizo zimekuwa ngumu kwa sababu ya milima na mabonde.
Miaka mitano iliyopita ndege iliyokuwa imebeba waruka mwavuli ilianguka baada ya kupaa angani kutoka Fox Glacier na kuwaua watu tisa.

No comments:

Post a Comment