Mkaazi mmoja wa ngome kuu ya wapiganaji wa Islamic State huko Syria katika jiji la Raqq ameambia BBC kuwa hali ya kibinadamu imezorota sana.
Mkaazi huyo, ambaye ni mwanachama wa kundi linalopinga Islamic State, ambaye hakutaka jina lake kutajwa, alisema kuwa mashambulizi ya mara kwa mara ya ndege za kijeshi tangu uvamizi wa Paris, Ufaransa, yamesababisha raia wengi kufariki na wengine kujeruhiwa.
Alisema kuwa eneo kubwa la mji huo halina umeme na kuwa watu wanaotumia mitandao hawawezi tena kufanya hivyo.
Ilikuwa vigumu kwa raia kuondoa Raqqa kwa kuwa ni wanachama wa Islamic State pekee wanaoruhusiwa kuingia na kuondoka kupitia vizuizi vilivyoko vinavyozunguka mji wote.
No comments:
Post a Comment