Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru akizungumza na Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha (hawapo pichani) kabla ya kufunga Mafunzo ya siku nane ya Uwezeshaji kwa wawezeshaji hao jana Jijini Mwanza. Kushoto ni Afisa Vijana Bw. Godfrey Massawe na kulia ni Mwezeshaji Kitaifa Bibi. Octavina Kiwone.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru akitoa cheti cha kuhitimu Mafunzo ya Uwezeshaji wa Stadi za Maisha kwa Bw. Edwin Gacho (kushoto) wakati wa kufunga Mafunzo hayo, jana Jijini Mwanza.
Ofisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Diana Kasonga (kushoto) akifuatilia Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha kutoka Mkoa wa Kagera wakiandaa Mpango kazi watakaotumia wakati wa kufikisha ujuzi walioupata kwa waelimisha rika wa Mkoa wa Kagera.
Mwezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha Bi. Virginia Chacha (kulia) akifanya mazoezi ya uwezeshaji kwa wawezeshaji wenzake kama njia mojawapo ya kupima uwezo wa wawezeshaji hao kabla ya kufunga Mafunzo ya Uwezeshaji jana Jijini Mwanza.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan
Ndunguru (wapili kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na Wawezeshaji wa
Kitaifa wa Stadi za Maisha baada ya kufunga mafunzo ya uwezeshaji jana Jijini
Mwanza. Wapili kulia ni Mtaalam wa Stadi za Maisha Bw. Benny Lugoe na wakwanza
kulia ni Afisa Vijana Bw. Godfrey Massawe.(Picha zote na Genofeva Matemu – Maelezo, Mwanza)
Na Genofeva Matemu - Maelezo, Mwanza
VIJANA wametakiwa
kutumia vizuri mazingira wanayowazunguka kuibua mbinu mbalimbali za
ujasiriamali ili kuweza kuondoka na taifa tegemezi kwa kusubiri kuajiriwa mara
baada ya kuhitimu masomo yao.
Rai hiyo imetolewa na
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru alipokua akifunga
mafunzo ya Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha jana Jijini Mwanza.
Bibi. Ndunguru
amesema kuwa vijana waliopata mafunzo ya uwezeshaji wa stadi za maisha ni
mabalozi ambao kama watatumia vizuri uwezo walioupata katika mafunzo hayo
watabadili fikra za vijana wengi nchini hivyo kuweza kujenga taifa lenye afya
nzuri, weledi na pamoja na ujuzi.
Kwa upande wake Mtaalamu
wa masuala ya Stadi za Maisha Bw. Benny Lugoe amesema kuwa washiriki wa Mafunzo ya Stadi za Maisha wana
ari na motisha ya kujifunza na kama wataendelea kuwa na ari hiyo watakua
wabunifu na wawezeshaji wazuri kwa vijana ndani ya jamii.
Aidha Bw. Lugoe amewataka wahitimu wa kitaifa wa
Stadi za Maisha kutimiza wajibu wao kwa kuwaandaa waelimisha rika katika mikoa
yao ili kuweza kutimiza malengo yaliyokusudiwa na kuweze kubadili fikra za
vijana katika jamii.
Naye Mwezeshaji wa
Kitaifa wa Stadi za Maisha kutoka Mkoa wa Shinyanga Bw. Ezra Manjerenga amesema
kuwa ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ni tatizo kubwa kwa Mkoa wa
Shinyanga hivyo ugeni wa mafunzo ya stadi za maisha katika Mkoa huo utawavutia
vijana wengi jambo ambalo litapelekea kutimiza lengo la serikali kufikisha
mafunzo hayo kwa vijana wa rika mbalimbali.
Bw. Manjerenga
ameiomba serikali kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wawezeshaji wa kitaifa wa
Stadi za Maisha haswa pale panapokua na mabadiliko katika mwongozo wa Stadi za
maisha ili kuweza kubadilisha fikra za vijana wote nchini.







No comments:
Post a Comment