Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya usafiri wa ndege ya Skylink travel & Travel, Moustafa Khataw, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa kuchezeshwa bahati nasibu ya wateja wa kampuni hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa wa Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed, wapili kulia ni Meneja wa Emirates nchini, Husain AlSafi na wapili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha wateja wa wadogo wadogo wa Benki ya Exim, Agnes Kaganda. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Meneja wa Emirates nchini, Husain AlSafi, akizungumza wakati wa uchezeshwaji wa bahati nasibu hiyo, ambayo washindi wanne walipatikana na kujinyakulia zawadi, zikiwemo magari mawili aina ya Hyundai.
Mkuu wa Kitengo cha wateja wa wadogo wadogo wa Benki ya Exim, Agnes Kaganda, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwakilishi wa Mahindra Holiday, Sagar Mehta (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha wateja wa wadogo wadogo wa Benki ya Exim, Agnes Kaganda, akikata utepe kuzindua bahati nasibu hiyo, kabla ya kuchezeshwa jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa wa Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed, akichanganya kuponi kabla ya kuanza kuchaguliwa washindi wa bahati nasibu hiyo, ya Skylink.
Mwakilishi wa Mahindra Holiday, Sagar Mehta (kulia), akichanganya kuponi kabla ya kuchagua moja kumpata mmoja wa washindi wa bahati nasibu hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya usafiri wa ndege ya Skylink travel & Travel, Moustafa Khataw (kushoto) na Mwakilishi Mahindra Holiday, Sagar Mehta (kulia) pamoja na Ofisa wa Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed (wapili kulia), wakiangalia tiketi ya mshindi wa kwanza wa gari wa bahati nasibu ya skylink, iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam leo. Watatu kulia ni Meneja wa Emirates nchini, Husain AlSafi.
Ofisa wa Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed, akiandika namba za mmoja wa washindi wa bahati nasibu hiyo, ya Skylink.
Meneja wa Emirates nchini, Husain AlSafi, akichanganya kuponi kabla ya kuchagua moja kumpata mmoja wa washindi wa bahati nasibu hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha wateja wa wadogo wadogo wa Benki ya Exim, Agnes Kaganda, akichagua moja ya kuponi za washindi wa bahati nasibu hiyo.
Mpigapicha wa TBC, Eva Sesoa, akichagua moja ya kuponi za washindi wa bahati nasibu hiyo.
Mpigapicha wa TBC, Eva Sesoa, akimkabidhi Ofisa wa Michezo ya Kubahatisha nchini, Abdallah Hemed moja ya kuponi za washindi wa bahati nasibu hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Safari za Nje wa Kampuni ya Skylink, Solomon Mwale, akizungumza na mmoja wa washindi wa bahati nasibu hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Safari za Nje wa Kampuni ya Skylink, Solomon Mwale, akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokuwa akitoa taarifa ya matokeo ya bahati nasibu hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Safari za Nje wa Kampuni ya Skylink, Solomon Mwale, akizungumza na mmoja wa washindi wa gari wa bahati nasibu hiyo.

No comments:
Post a Comment