TANGAZO


Tuesday, September 15, 2015

CCM Zanzibar yazindua kampeni Kisiwani Pemba Uwanja wa Gombani ya Kale leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akiwa Mgombea wa Urais wa kupitia CCM kwa kipindi cha pili Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar wakipeperusha bendera wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za CCM katika Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chekechake Mkoa wa Kusini Pemba leo. (Picha zote na Ikulu)
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), waliohudhuria katika Ufunguzi wa Kampeni za CCM katika Mkoa wa Kusini Pemba, zikiongozwa na Mgombea Urais kwa kipindi cha pili Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika Uwanja wa Gombani ya kale Wilaya ya Chake Chake.
Baadhi ya WanaCCM na wananchi waliofurika katika Uwanja wa Gombani ya kale Wilaya ya Chake chake leo kusikiliza sera za Chama cha Mapinduzi katika uzinduzi wa Kampeni za CCM kugombea nafasi ya Urais,Ubunge na Udiwani zinazoongozwa na Mgombea wa Urais wa kupitia CCM kwa kipindi cha pili Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Ufunguzi wa kampenzi za CCM zilizofanyika leo katika uwanja wa Gimbani yakale Wilaya ya chakechake Pemba.
Mgombea Urais kwa kipindi cha pili,Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akionesha ilani ya chama wakati wa Mkutano wa Hadhara wa ufunguzi wa Kampeni za Chama hicho katika Uwanja wa Gombani ya kale Wilaya ya Chakechake Pemba leo.

No comments:

Post a Comment