TANGAZO


Sunday, August 16, 2015

Vita vya Iraq:Bush na Clinton walaumiana

Clinton na Jeb Bush
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Demokrat Hillary Clinton amemshtumu mpinzani wake kutoka chama cha Republican Jebb Bush kuhusu ni nani aliyesababisha msukosuko nchini Iraq.
Siku ya jumanne bwana Bush aliishtumu serikali ya rais Obama kwa kuyaondoa mapema majeshi ya Marekani mwaka 2011 swala analosema limesababisha madhara makubwa.
Lakini Bi Clinton alijibu kwa kusema ni nduguye George W Bush ambaye aliomba majeshi ya Marekani kuondolewa nchini humo.
Vita vilivyoanzishwa na Marekani nchini Iraq mwaka 2003 vimesababisha msukosuko nchini humo.
Bwana Bush alisema kuwa kuondolewa kwa vikosi vya Marekani nchini Iraq ilikuwa makosa yaliosababisha maafa makubwa ikiwemo msukosuko na hatimaye kuanza kwa kundi la wapiganaji wa Islamic State.
''Walitaka kuwa katika kumbukumbu za kihistoria badala ya kuleta amani'',Bwana Bush alisema akimshtumu rais Obama na Bi Hillary Clinton wakati Clinton alipokuwa katibu wa maswala ya kigeni mwaka 2009 na 2013.

No comments:

Post a Comment