TANGAZO


Thursday, August 13, 2015

Simba yakabidhi zawadi kwa washindi wa bahati nasibu ya Simba Day

Rais wa Simba, Evans Aveva, akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni, zawadi ya mpira, Dar es Salaam leo,  baada ya kuibuka mmoja wa washindi katika bahati nasibu ya Siku ya Simba iliyochezeshwa wakati wa tamasha lakuwatambulisha wachezaji wapya wa Simba, Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAGgroup, Imani Kajula. (Picha na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Na Mwandishi wetu KLABU ya Simba leo tarehe 13 – 8 – 2015 imekabidhi zawadi za washindi wa bahati nasibu iliyofanyika siku ya Simba Day, ambapo washindi walipata Simu za mkononi, jezi, vifaa vya michezo na mavazi mbalimbali yenye chapa Simba. 

Katika halfa hiyo ambayo Rais wa Klabu ya Simba Evans Aveva alikuwa mgeni rasmi, alisema “klabu ya Simba ni klabu inayojali na kuwathamini wapenzi, wanachama na wadau wote wa Simba na ndio maana kila wakati inabuni njia za kuonesha kuthamini kwa mchango wao katika maendeleo ya klabu”.

Leo pia klabu ya Simba ilikabidhi vifaa vya michezo katika shule mbalimbali ili kuweza kukuza vipaji vya watoto mashuleni kwani michezo ni sehemu ya afya na ili mtoto aweze kufanya vizuri shuleni ni lazima awe na afya bora. Lakini pia tunaamini hii ndio njia bora zaidi ya kuchochea vijana kupenda mpira hivyo kukuza vipaji.

Simbasports.co.tz ilipata nafasi ya kuongea na mmoja wa washindi na kuzungumzia furaha yake siku ya leo Marko Samwely Mgimba “nimefurahi sana tena sana, sikutegemea kuwa ni kweli nitapata hii zawadi yangu nilijua kuwa ndio basi nimekosa zawadi yangu lakini leo nashukuru sana klabu yangu ya Simba kwa kuwa wakweli na kutimiza ahadi zao wanazotupatia lakini pia kwa kutujali wanachama na wapenzi wa Simba, nashukuru sana Uongozi wa Simba kwa kuwa karibu na wapenzi na wanachama wake”.

Simbasports.co.tz pia ilipata nafasi ya kuongea na Mwalimu wa shule ya Chang’ombe Mwl. Ishengoma na kusema “naishukuru sana klabu ya Simba kwa kuthamini umuhimu wa michezo mashuleni lakini pia kuona umuhimu wa kutoa vifaa ya michezo katika shule yetu, kwa niaba ya shule yangu tunaishukuru sana klabu ya Simba kwa zawadi hizi”.

Simbasports.co.tz inaupongeza Uongozi wa Simba kwa kuwa karibu sana na jamii inayoizunguka klabu yetu na kuonesha kuthamini kwa mchango wao katika maendeleo ya klabu ya Simba. SIMBA NGUVU MOJA.

No comments:

Post a Comment