TANGAZO


Saturday, August 15, 2015

Simba yaipiga URA ya Uganda mabao 2-1 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Wanachama na mashabiki wa Simba, wakiwa kwenye Uwanja wa Taifa, kungalia mchezo wa kirafiki wa Kimataifa, baina ya timu hiyo, na URA ya Uganda, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)   
Ubao wa matokeo ukisomeka Simba 0 Vs URA 0, kabla ya mchezo kati ya timu hizo leo, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu za Simba ya Tanzania na URA ya Uganda wakiingia uwanjani tayari kuanza mpambano huo.
Wachezaji wa timu za Simba ya Tanzania na URA ya Uganda wakiingia uwanjani kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati yao.
Wachezaji wa timu za Simba ya Tanzania na URA ya Uganda wakisalimiana kabla ya kuanza mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa. 
Wachezaji wa Simba wakipiga picha ya kumbukumbu ya mchezo huo. 
Wachezaji wa URA ya Uganda, wakipiga picha ya kumbukumbu ya mchezo huo.  
Benchi la ufundi na wachezaji wa akiba wa URA ya Uganda, likiongozwa na Kocha Moses Basena (kulia), wakati wa mchezo huo.
Benchi la ufundi na wachezaji wa akiba wa Simba ya Tanzania, likiongozwa na Kocha Dylan Kerr (kushoto) wakati wa mchezo huo.
Mchezaji Kelvin Ndayisenga wa Simba, akipiga mpira uliombabatiza Kasozi Bob wa URA ya Uganda (kushoto), katika mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilimeshinda mabao 2-1.
Mchezaji Kelvin Ndayisenga wa Simba, akishangilia, baada ya kuipatia timu yake hiyo, bao la kwanza dhidi ya URA ya Uganda katika mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. 
Kelvin Ndayisenga, akikumbatiana na wachezaji wenzake wa Simba, wakati wakishangilia bao la kwanza aliloifungia timu yake hiyo, dhidi ya URA ya Uganda katika mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa.
Wachezaji wa Simba, wakishangilia bao hilo, lililofungwa Kelvin. Katika mchezo huo, Simba ilishinda mabao 2-1. 
Ubao wa matangazo ukionesha Simba bao 1 na URA ya Uganda 0.
Ubao wa matangazo ukionesha Simba bao 1 na URA ya Uganda 1, baada ya URA kufanikiwa kusawazisha bao hilo.
Mchezaji Kagimu Sadiq wa URA ya Uganda, akimkwatua Samih Ali Nuhu wa Simba, wakati wa mchezo huo, wa kirafiki wa Kimataifa, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. 
Awadh Juma wa Simba akiruka na mlinda mlango wa URA, Bwete Brian kuuwahi mpira uliokuwa ukiwaniwa na Massa Simeon (17) wa URA.
Kocha wa Simba, Dylan Kerr, akizungumza na wachezaji wake wakati wa mapumziko kabla ya kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. 
Wanachama na mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo huo.
Massa Simeon wa URA, akikimbia na mpira huku akifuatwa na Kelvin Ndayisenga (nyuma) wa Simba.
Massa Simeon wa URA, akimtoka Kelvin Ndayisenga wa Simba.
Mussa Hassan Mgosi wa Simba akiuzuiya mpira huku akifuatwa na wachezaji wa URA. 
Mussa Hassan Mgosi wa Simba akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Kagimu Sadiq wa URA. 
Hassan Kessy wa Simba kijaribu kumpiga chenga Sekito Sam (13) wa URA. 
Ibrahim Ajib (kushoto) na Juuko Murshad wote wa Simba wakishangilia bao la pili lililofungwa na Juuko na hivyo Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo huo.
Ibrahim Ajib (kushoto) na Juuko Murshid wote wa Simba wakishangilia bao hilo la pili lililofungwa na Juuko Murshid
Wachezaji wa Simba wakifurahia bao hilo. 
Hassan Is-haka akimkumbatia kwa furaha Juuko Murshid baada ya Murshad kuifungia timu yao ya Simba bao la pili katika mchezo huo, dhidi ya URA ya Uganda iliyopata bao 1.
 Ubao wa matangazo ukionesha Simba 2 na URA 1.
Mussa Hassan Mgosi wa Simba akipambana na wachezaji wa URA.
Mussa Hassan Mgosi wa Simba akiwatoka wachezaji hao wa URA.
Hadi mwisho wa mchezo huo, ubao wa matangazo ulikuwa ukionesha Simba 2 na URA 1.

No comments:

Post a Comment