Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Semfue
Na
Lorietha Laurence-Maelezo
SERIKALI ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania imefanikiwa
kumiliki kiwanda cha kutengeneze magurudumu ya magari cha General Tyre kwa
asilimia 100 baada ya kununua hisa 26 zenye thamani ya dola milioni moja kutoka
kwa Kampuni ya Continental AG.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika Ofisi ya Msajili wa Hazina wakati wa makabidhiano ya nyaraka za ununuzi
wa hisa hizo, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Semfue anasema jitihada za
kuhakikisha kuwa serikali inamiliki hisa hizo
zilianza tangu mwaka 2012 kwa kufanya mazungumzo ya awali na mwekezaji.
“Kufuatia hatua hii ya
kuweza kumiliki hisa kwa asilimia 100 sasa tutakuwa na fursa ya kuzalisha
magurudumu yetu wenyewe na hivyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa
kikitumia kununua magurudumu kutoka nje” alisema Balozi.Semfue.
Aidha anaendelea
kufafanua kuwa hatua itakayofuata ni kutamfuata mwekezaji atakayeshirikiana na
Shirika la Maendelao la Taifa (NDC) katika kuzalisha magurudumu kwa kutumia teknolojia
ya kisasa.
Balozi.Semfue anampongeza Rais Mhe. Jakaya Kikwete kwa
kufanikisha zoezi zima la kuhakikisha serikali inamiliki hisa za kiwanda cha General Tyre kwa asilimia
100 na hivyo kufufua uchumi wa jiji la Arusha na Taifa kwa ujumla.
Naye Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru anasema mpaka serikali kuweza
kumiliki hisa hizo ni hatua kubwa sana kutokana na vikwazo mbalimbali
vilivyokuwa vikiwekwa na mwekezaji wa kiwanda hicho kilichoanzishwa mwaka 1969.
“Haikuwa kazi rahisi
kumiliki hisa hizi bila ya jitihada kubwa iliyofanywa na serikali katika kumshawishi mwekezaji baada ya kuona
hana kuwa hakuwa tayari kuwekeza na hivyo kurejesha umiliki kwetu” alisema
Mafuru.
Kwa upande wa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Uledi Musa, anaeleza kuwa kiwanda
hicho kitatoa fursa za ajira zaidi kitakapoanza kuzalisha tofauti na awali
ambapo kiliweza kuajiri wafanyakazi 360.

No comments:
Post a Comment