Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema ''presha ni kubwa'' katika mchezo wa jummane dhidi ya Club Brugge katika hatua ya mtoano ligi ya mabingwa ulaya.
Mashetani hao wekundu watakawakaribisha timu hiyo kutoka Ubelgiji kabla ya mchezo wa pili ambapo mshindi ataingia katika hatua ya makundi. Van Gaal, aliyeanza kuinoa Man U mwaka 2014, anatazamiwa kuiongoza Man U kurudi katika michuano ya Ulaya tokea msimu wa 2013-2014.
''Huwezi kusema kuwa huna presha, wao pia ni timu nzuri'' alisema''Tunapaswa kuonyesha ubora wetu'' United wataingia katika mchezo huo wakitaka kuendeleza rekodi yao ya ushindi tokea msimu huu kuanza baada ya kuwashinda Totenham na baadae Aston Villa kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Nahodha timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney amekua akiiongoza vema Man U tokea kuanza kwa msimu licha ya kuwa bado hajafumania nyavu. Van Gaal anaamini kuwa muda sio mrefu Rooney ataanza kufumania nyavu.
No comments:
Post a Comment