*Chini: Picha za matukio mbalimbali za uzinduzi wa kampeni za CCM viwanja vya Jangwani
Baadhi ya wanachama na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni mgombea wa Urais wa chama hicho, Dk. John Pombe Magufulli, viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) Walinzi wa Chama wakizuia umati wa wanachama na wananchi waliokuwa wamejazana na kusukumana kutaka kusimama katika nafasi za mbele kwenye mkutano huo jijini leo.
Umati wa wanachama na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni mgombea wa Urais wa chama hicho, Dk. John Pombe Magufulli, viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam leo.
Waziri Januari Makamba akiwasili.
Mabasi ya mgombea wa CCM, Dk. Magufuli yakiingia uwanjani.
Basi lililobeba wasanii likiingia uwanjani.
Waziri Kiongozi mstaafu, Nahodha akiingia Uwanjani.
Kundi la Tanzania One Theatre (TOT), likitumbuiza.
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi akiingia uwanjani.
Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki alipokuwa akiingia uwanjani kwenye uzinduzi huo.
Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, akiingia uwanjani kwenye uzinduzi huo.
Waziri Mkuu wastaafu, Jaji Joseph Warioba na Dk. Salim Ahmed Salim wakiingia uwanjani kwenye uzinduzi huo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa akiingia uwanjani katika mkutano huo.
Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal akiingia kwenye viwanja vya Jangwani wakati wa uzinduzi huo.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiingia kwenye viwanja vya Jangwani wakati wa uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais, Jakaya Kikwete akiingia kwenye viwanja vya Jangwani wakati wa uzinduzi huo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiingia kwenye viwanja hivyo wakati wa uzinduzi huo.
Mbunge wa Chalinze mkoani Pwani, Ridhwan Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema wakati alipowasili kwenye viwanja hivyo katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida kwenye viwanja hivyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili viwanjani hapo.
Mgombea wa nafasi ya Urais, Dk John Magufuli na mgombea mwenza wake, Samia Suluhu Hassan wakiwapungia wanachama walipowasili viwanjani hapo tayari kwa uzinduzi leo.
Mgombea wa nafasi ya Urais, Dk John Magufuli na mgombea mwenza wake, Samia Suluhu Hassan wakiwapungia wanachama walipowasili viwanjani hapo tayari kwa uzinduzi leo.
Dk. Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema alipowasili viwanjani hapo.
Mgombea wa nafasi ya Urais, Dk John Magufuli akiwapungia wanachama alipowasili viwanjani hapo tayari kwa uzinduzi leo.
Mgombea wa nafasi ya Urais, Dk John Magufuli akiwapungia wanachama alipowasili viwanjani hapo tayari kwa uzinduzi leo.
Mgombea wa nafasi ya Urais, Dk John Magufuli na mgombea mwenza wake, samia Suluhu Hassan wakiwapungia wanachama walipopanda kwenye jukwaa tayari kwa kukabidhiwa Ilani ya chama hicho.
Mgombea wa nafasi ya Urais, Dk John Magufuli na akimkumbatia Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Mgombea wa nafasi ya Urais, Dk. Pombe Magufuli (kulia), akimshukuru Rais Jakaya Kikwete
Mgombea wa nafasi ya Urais, Dk. Pombe Magufuli (kulia), akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheina.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete na mgombea wa nafasi ya Urais, Dk. Pombe Magufuli wakifurahia jambo.
Meza Kuu wakiimba waimbo wa Taifa.
Wasanii wa Yamoto Band wakitumbuiza katika mkutano huo.
Kada wa CCM, mlemavu wa macho, Amon Mpanju akihutubia katika mkutano huo.
Umati wa wanachama na washabiki wa CCM, wakiwa katika mkutano huo.
Makongoro Nyerere akihutubia katika uzinduzi wa kampeni hizo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete na mgombea wa urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli wakicheza wimbo wa TOT, wakati wa uzinduzi huo.
Msanii Nasib Abdul 'Diamond Platnamuz' akitumbuiza katika uzinduzi wa kampeni za CCM leo.
Msanii Nasib Abdul 'Diamond Platnamuz' akitumbuiza katika uzinduzi wa kampeni za CCM leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano huo.
Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Sinde Warioba akihutubia katika mkutano huo.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Shein akihutubia mkutano huo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akihutubia katika uzinduzi huo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, akihutubia katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akihutubia mkutano huo, wakati akizindua rasmi kampeni za chama hicho, leo viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akihutubia mkutano huo, wakati akizindua rasmi kampeni za chama hicho, leo viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete, akimkabidhi Ilali ya uchaguzi mgombea wa nafasi ya Urais, Dk John Magufuli.
Mgombea wa nafasi ya Urais, Dk John Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini leo.
Mgombea wa nafasi ya Urais, Dk John Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini leo.
Mgombea wa nafasi ya Urais, Dk John Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini leo.





No comments:
Post a Comment