TANGAZO


Thursday, May 7, 2015

Yemen:Saudia yapendekeza kusitisha Vita

Kampeini hiyo ya vita vya hewani imedumu kwa muda wa majuma 6.
Saudi Arabia inasema inajiandaa kufanya mashauriano ya siku tano ya kuleta amani na kujiondoa kutoka katika operesheni ya majuma 6 nchini Yemen kwa sababu ya kibinadamu.
Hayo yametangazwa baada ya mazungumzo na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani John Kerry.
Hatua hiyo ya Saudi Arabia inafanyika baada ya mashambulio makali ya angani kutoka kwa ndege za majeshi ya Saudia kwa pamoja na majeshi ya muungano, ya kukabiliana na wapiganaji wa huthi huko Yemen.
Aidha Saudi Arabia inasema pia kuwa waasi hao wa kishia pia wanafaa kusitisha mapigano na kuweka silaha chini.
Saudia imetekeleza mashambulizi nchini Yemen kwa nia ya kuwashurutisha wapiganaji wa Kiislamu wa kabila la Wa-Houthi kusitisha kampeini yao dhidi ya rais aliye uhamishoni Abdrabbuh Mansour Hadi.
Kwa mujibu wa duru za umoja wa mataifa takriban watu 1400 wameuawa.
Hadi alitoroka Yemen mwezi februari alipozidiwa na wanamgambo hao akitokea mji wa Aden.
Kampeini hiyo ya vita vya hewani imedumu kwa muda wa majuma 6.
Kwa mujibu wa duru za umoja wa mataifa takriban watu 1400 wameuawa.

No comments:

Post a Comment