Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akihutubia kwenye dhifa.
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi akizungumza.
Baadhi ya Maofisa Balozi waliohudhuria dhifa wakibadilishana mawazo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi na wageni waalikwa katika hafla hiyo. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Julieth Kairuki.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye na Mbunge wa Singida Mjini (CCM) Mohamed Dewji na Mfanyabiashara Maarufu nchini Yusuph Manji.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya viongoz wa Serikali ya Msumbiji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na Mnadhimu Mku wa Majeshi , Samuel Ndomba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati mwenye tai nyekundu) akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakifurahia burudani ya kikundi cha ngoma baada ya kumalizika kwa dhifa ya Kitaifa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, akumuongoza mgeni wake kutoka nje ya ukumbi wa Ikulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Kikwete, akimuaga mgeni wake. (Picha na
Hussein Makame-MAELEZO)
Na Magreth Kinabo – Maelezo
TANZANIA na Msumbiji zimekubaliana kushirikiana kiuchumi, ili kuweza kuboresha hali ya uchumi kwa manufaa ya nchi hizo pamoja na watu wake.
Hayo yalisemwa jana wakati wa hafla ya dhifa ya kitaifa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaama ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alimuandalia mgeni wake Rais wa Msumbuji Mhe. Filipe Nyusi.
Akizungumzia kuhusu ziara yake Rais Nyussi alisema kuwa amefurahishwa na mapokezi aliyoyapata na kuongeza kwamba ujio huo utaendeleza ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi hizo mbili kupitia nishati ya gesi.
“Nina imani kwamba tutaweza kushirikiana kiuchumi ili kuendeleza ushirikiano wetu hususani kupitia nishati ya gesi,” alisema Rais Nyusi.
Rais Nyusi aliongeza kwamba ili kuweza kupata mafanikio ya kiuchumi zaidi upo umuhimu wa kuimarisha viwanda kwa kuvisaidia viwanda vya kati na vidogo.
Kwa upande wake Rais Kikwete alisema ujio wa Rais Nyusi ni ishara ya kuingia katika hatua nyingine ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili kutokana na kwamba wamekubaliana kushirikiana katika utoaji visa , masuala ya kiuchumi kupitia gesi, kielimu, ulinzi na usalama , ikiwemo kuendeleza biashara na uwekezaji .
Rais Kikwete aliongeza kuwa anatarajia kumaliza muda wa uongozi wake huku uhusiano wa nchi hizo ukiwa katika hali nzuri na anatagemea kwamba utaendelea kuwa imara hata atakapomaliza muda wake.
Rais Nyusi yupo hapa nchini kwa ziara yake ya siku tatu ikiwa ni ya kwanza kuifanya nchi za nje tangu alipochaguliwa kushika madaraka ya nchi hiyo.














No comments:
Post a Comment