Mabondia Adam Ngange wa Chanika, Dar es Salaam (kushoto) na Iddi Pialali wa Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, wakioneshana umwamba kwa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Chuo cha Sanaa, Bagamoyo (TASUBA). Ngange alishinda kwa point mpambano huo wa raundi sita (Picha zote na Super D)
Bondia Adam Ngange (kushoto), akimpiga konde la kulia bondia Iddi Pialala, wakati wa mpambano huo.
Bondia Iddi Pialali, akimtupia makonde mfululizo bondia Adam Ngange.Na Mwandishi Wetu
BONDIA Adam Ngange wa Chanika Dar es Salaam amemsambaratisha Iddi Pialali wa Kiwangwa, Bagamoyo kwa pointi katika mpambano wao mkali wa raundi sita, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA), mwishoni mwa wiki iliyopita.
Pilikapilika za furaha ziliufunika ukumbi huo wakati wa mpabano huo wa raundi sita.
Walikuwa ni mashabiki wa bondia Adam Ngange waliotoka na furaha baada ya kumsambaratisha mpinzani wake kwa pointi.
Mambambano kati ya mabondia hao, ulianza taratibu kabla ya kupamba moto kadiri muda na raundi zilivyokuwa zikisonga mbele.
Bondia Pialali alimshambulia mpinzani wake Ngange kwa kasi katika raundi za mwanzo, lakini kadri mpambano ulivyokuwa ukisonga mbele kasi yake ilipungua na hivyo kumpa mwanya mpinzani kutamba zaidi kwenye raundi za mwisho.
Bondia Ngange alijitahidi kujitutumua na kumwachia ngumi za haraka na nzito mpinzani wake huyo, ambaye naye alijitahidi kuvumilia mashambulizi hayo hadi zipomalizika zote sita na hivyo bondia huyo kuibuka na ushindi wa pointi.

No comments:
Post a Comment