TANGAZO


Thursday, May 21, 2015

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu atatua mgogoro wa mikataba ya wananchi wa Mtaa wa Chaurembo Kurasini jijini Dar es Salaam

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Wavuvi, Mtaa wa Chaurembo, uliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam, baada ya kutokea mwekezaji na kusababisha sintofahamu ya muda mrefu na kupelekea wananchi kufanya maandamano ya amani hadi Ofisi za Serikali ya mtaa huo na kumlazimu Mbunge kuingilia kati mgogoro huo. (Picha zote na Khamisi Mussa)
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu, akipitia moja ya mkataba waliyoandikiwa wananchi hao na mwekezaji, ambayo wananchi hao hawajaridhishwa nayo. Kushoto ni Muhandisi Msaidizi wa Bandari  na kiongozi wa kero za wananchi wa kijiji Chawavuvi Mtaa wa Chaurembo, Kurasini, David Mlassi akimweleza jambo fulani mbunge huyo.
Wananchi wa Kijiji cha Wavuvi, Mtaa wa  Chaurembo jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza Mbunge huyo.
Wananchi wa Kijiji wa Chaurembo, wakipiga makofi baada ya  Mbunge huyo kuongea jambo.
Wananchi hao, wakimsikiliza  kwa makini mbunge wao huyo, alipokuwa akizungumza jambo.
Wananchi wakiimba na kufurahi baada ya Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu, kusikiliza na kutatua kero zao.
Ilikuwa ni furaha kwenda mbele, baada ya kutatuliwa matatizo yao hayo. 

No comments:

Post a Comment