*Akutana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Serikali ya China, wakati alipowasili kwenye ukumbu Maalum wa watu wa China, 'Peoples Great Hall' kwa ajili ya mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo, jana Mei 20, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakisimama kwa heshima wakati zikipigwa nyimbo za Taifa la Tanzania na China, kwenye mapokezi yake katika Ukumbi Maalum wa Watu wa China, kwa ajili ya mazungumzo baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Nchina.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati akikagua gwaride la heshima kwenye Ukumbi Maalum wa watu wa China, Peoples Great Hall, wakati alipofika kwa mazungumzo na mwenyeji wake baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati akikagua gwaride la heshima kwenye Ukumbi Maalum wa watu wa China, Peoples Great Hall, wakati alipofika kwa mazungumzo na mwenyeji wake baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati akikagua gwaride la heshima kwenye Ukumbi Maalum wa watu wa China, Peoples Great Hall, wakati alipofika kwa mazungumzo na mwenyeji wake baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ujumbe wake (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao na ujumbe wake (kulia) kwenye Ukumbi maalum wa Watu wa China, 'Peoples Great Hall' baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini China.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ujumbe wake (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao na ujumbe wake (kulia) kwenye Ukumbi maalum wa Watu wa China, 'Peoples Great Hall' baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini China.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisindikizwa na mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya mazungumzo yao kwenye Ukumbi Maalum wa Watu wa China, jijini Beijing China. Kushoto ni mkarimani wa Makamu wa Rais wa China.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya mazungumzo yao kwenye Ukumbi Maalum wa Watu wa China, jijini Beijing China. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini China.
Na Ofisi ya Makamu wa Rais
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Jumatano Mei 20, 2015
alimalizia ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini China ambapo amekutana na
mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China Mheshimiwa Li Yuanchao na kupata mapokezi
Rasmi ya Serikali ya China katika ‘Ukumbi Maalum’ kwa wa Watu wa China.
Makamu
wa Rais katika mapokezi hayo alipata nafasi ya kukagua gwaride na kisha
kuongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais Yuanchao katika ukumbi wa
mazungumzo.
Makamu wa Rais wa China
alitumia nafasi hiyo kumshukuru Makamu wa Rais wa Tanzania kwa kukubali mwaliko
wake na hivyo kufanya ziara ya kikazi nchini China na pia akaongeza kuwa,
uhusiano wa China na Tanzania ni wa wakati wote na akasisitiza kwamba
ushirikiano baina ya nchi hizi mbili unatoka katika mioyo ya wananchi.
“Nilipokuwa
Tanzania mwaka jana mwezi wa Juni niliona namna raia wa China anavyothaminiwa
na kuheshimiwa nchini Tanzania. Jambo hili lilinipa furaha na kunielimisha
kuhusu nchi zetu,” Makamu wa Rais Yuanchao alisema.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal
alitumia nafasi hiyo licha ya kushukuru kwa Mwaliko pia kuzungumzia agenda za
maendeleo ya Tanzania huku akisisitiza kuwa, anayo furaha kuhusu kukamilika kwa
usimikaji wa mkondo wa Taifa kwa awamu zote mbili huku akiitaka serikali ya
China kuendelea kuwa na Tanzania katika kukamilisha awamu ya tatu, jambo ambalo
Makamu wa Rais Yuanchao alilikubali.
Mheshimiwa Makamu wa Rais
Dkt. Bilal alizungumzia pia ziara yake katika majiji ya Wuhan na Nanjing na
akaelezea furaha yake kuhusu namna wananchi wa China wanavyoitazama Tanzania na
namna walivyo tayari kushirikana nayo katika kukuza maendeleo ya viwanda
sambamba na kutanua soko la biashara baina ya Tanzania na nchi zinazoizunguka.
Pia alipata nafasi ya kuzungumzia kuhusu namna ya kuboresha reli ya TAZARA huku
akimtaka Makamu wa Rais Yuanchao kusaidia kwa kuwaita Mawaziri wa Uchukuzi toka
Zambia na Tanzania ili wakutane na wenzao wa China ili kuhakikisha kunapatikana
mkakati mpya wa namna ya kuiendesha Reli hiyo kwa faida ya nchi washirika.
“Reli hii ni moja ya
viashiria vikubwa vya historia ya mahusiano yetu. Sisi Tanzania tusingependa
kuona inakufa,” alisema Makamu wa Rais Dkt. Bilal na kuongeza kuwa mazungumzo
kama hayo yanatakiwa kufanyika katika mradi wa ujenzi wa sehemu ya uwanja wa
ndege wa Zanzibar ambao umesimama ujenzi kufuatia pande mbili kushindwa
kuelewana.
Kwa upande wake Makamu wa
Rais wa China yeye aliihakikishia Tanzania kuwa China inao uzoefu mkubwa katika
mambo mengi hivyo Tanzania inatakiwa kutumia urafiki wake na China katika
kushirikiana kwenye masuala ya maendeleo.
Pia alifafanua kuwa serikali za
Tanzania, Oman na China zinatakiwa kuendelea kushirikana katika suala la Ujenzi
wa Bandario na Bagamoyo na kwamba serikali yake imejipanga kuendelea
kuwafadhili wanafunzi wa Kitanzania kusoma masomo ya Mafuta na Gesi.
“Wakati nilipokuwa Tanzania
nilifurahishwa na namna watu wenu wanavyoonesha uwezo wa kukabiliana na
changamoto za sasa. Watu hawa wanaweza kabisa kufanya kazi za aina mbalimbali
hivyo sisi tunaitazama Tanzania kama sehemu ya kuifanya Afrika itanuke na hivyo
uhusiano wa China na Afrika ubakie kama ulivyokuwa katika kipindi cha Afrika kutafuta uhuru,”
alisema.
Mheshimiwa Makamu wa Rais
amemaliza ziara yake na moja kwa moja kuanza safari ya kurejea nchini ambapo
anategemea kushiriki mikutano ya Chama cha Mapinduzi inayofanyika mjini Dodoma.
Katika ziara hiyo ya siku tatu nchini China, Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt.
Bilal aliambatana na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa
Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah
Kigoda na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali kutoka Zanzibar Mheshimiwa Ali
Juma Shamhuna.
Mwingine ni Naib u Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim.
Imetolewa
na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Mei
20, 2015
Beijing,
China
No comments:
Post a Comment