Wafanyabiashara wenye ulemavu wakiwa wamekaa katikati ya makutano ya Barabara za Uhuru na Kawawa na kufunga barabara hizo, wakipinga kubomolewa vibanda vyao vya biashara na Halmshauri ya Manispaa ya Ilala Dar es Salaam leo mchana. Halmshauri hiyo ilivunja vibanda hivyo kupisha upanuzi wa barabara.
Wananchi wakiwa eneo la tukio wakiwangalia wafanyabiashara hao walemavu walivyofunga barabara hizo.
Wafanyabiashara hao wakiwa wamekaa mbele ya malori wakizuia yasipite mpaka kieleweke.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akiwaeleza wafanyabiashara hao maafikiano yaliyofikiwa na viongozi wao.
Mmoja wa Wafanyabiashara hao, akizungumza kwa hisia kali katika tukio hilo.
Na Mwandishi wetu, Dar
WALEMAVU jijini Dar es Salaam, leo walilazimika kuifunga Barabara ya Kawawa na Uhuru zaidi ya saa sita baada ya kuvunjiwa vibanda pamoja na meza zao za biashara katika soko la Mchikichini.
Akizungumza leo, Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara walemavu, Kidumke Mohamed alisema leo, walipofika katika maeneo yao, ya kufanyia biashara walishangaa meza zao zaidi ya 200 pamoja na vibanda vyao vimevunjwa na mizigo yao ya biashara imechukuliwa.
Alisema hawajui kuwa ni nani aliyeharibu vitu vyao wakati Serikali iliwaruhusu kwa barua ya maandishi kufanya biashara katika soko hilo kuhu wakisubiri kutafutiwa eneo lingine.
Alisema kutokana na hali hiyo waliamua kuziba barabara kwa lengo la kupata suluhu kutoka kwa viongozi wa Serikali.
Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu, John Mleba, alisema kwa kuwa Serikali imeamua kuvunja Sheria ya makubaliano waliyokubaliana kwa njia ya maandishi wameamua kuvunja sheri.
Alisema hawawezi kuondoka wala kuruhusu barabara kupita hadi pale watakapopatiwa ufumbuzi juu ya kufanya biashara zao katika eneo hilo pamoja na kulipwa fidia ya vitu vyao vilivyoharibiwa.
“Hapa hatutoki mpaka Mkuu wa Mkoa Sid Meck aje kutatua tatizo hili kwani yeye ndiye aliyeturuhusu kufanya biashara katika soko hili tena makabuliano hayo yalitolewa kwa njia ya maandishi sasa tunashangaa wametufanyia hivi bila kutupatia taarifa.
“Wangetupatia taarifa mapema sisi tngeondoa vitu vyetu lakini wameviharibu na vingine wamevibeba wakati sisi tunapata fedha za kujikimu kimaisha kupitia biashara hizi,” alisema Mleba.
Mkuu wa Mkoa wa Ilala Raymond Mushi alifika katika eneo hilo kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro huo lakini walemavu hao walimfukuza na baadaye alifika OCD Mkoa wa Ilala ambaye naye pia walimfukuza.
Wakati barabara hiyo ikiendelea kufungwa na walemavu hao walikuwa wakiruhusu kupita gari za Jeshi la Kujenga Taifa(JWTZ) pamoja na Gari za kutolea huuma ya kwanza(Ambulance) huku gari za Polisi zipatazo nanae pamoja na askari lukuki walikuwa wamezingira katika eneo hilo.
Baada ya hapo Manispaa, Uongozi wa Wafanyabiashara Walemavu pamoja na Mkuu wa Wilaya walikaa kikao cha ndani ambapo chenye lengo la kusuluhisha mgogoro huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa lengo la kubomoa vibanda hivyo ni kupisha utanuzi wa barabara ya watembea kwa miguu katika eneo hilo.
Alisema kutokana na hali hiyo waliafikiana kwa njia ya maandishi kwa mara ya pili kuwa wenye uwezo warudi nawatengeneze meza zao nakuendelea kufanya biashara na wale wasiokuwa na uwezo wasubiri uchunguzi wa kutathmini athari zilizotokea ili walipwe fidia ya vitu vyao vilivyoharibika.
Pamoja na kupewa ahadi hiyo lakini wamewataka Serikali kuhakikisha kuwa ifikapo keshokutwa, tathimini hiyo iwe imeshakamilika ili watu waweze kulipwa fidia zao.
Hata hivyo walemavu hao wameitaka Serikali kuacha kuwa na tabia ya kigeugeu kwa ni hilo ni swala la aibu kwa jamii na taifa kwa ujumla na kuwaomba suala hilo lisijirudie tena.
Pia waliwaomba samahani wananchi wanaotumia barabara hiyo kwa usumbufu uliojitokeza na kushindwa kufanya shughuli zao kwa wakati.
Baada ya tamko hilo mnamo saa 10:30 jioni, Naibu Kamishna wa Polisi Kamanda Simon Siro, aliwaamuru askari wake kuruhusu magari yaliyokuwa yamezuiwa na walemavu hao kuendelea na safari zake.
No comments:
Post a Comment