Waziri mkuu wa Uingereza aliyechaguliwa kwa awamu ya pili David Cameron anatumia wikendi hii kukamilisha orodha yake ya mawaziri baada ya chama chake kushinda kwa uchaguzi mkuu nchini Uingereza.
Cameron tayari amemchagua Goerge Osborne ambaye tayari amefanywa kuwa waziri wa kwanza wa maswala ya kitaifa.
Theresa May,Phillip Hammond na Michael Fallon wataendelea kushikilia nyadhfa zao katika wizara ya maswala ya ndani,maswala ya kigeni na ulinzi huku matangazo mengine yakitarajiwa kufanywa siku ya jumatatu.
Wakati huohuo Vyama vya leba na Liberal Democrats vimeanza kuwatafuta viongozi wapya.
Ed Miliband na Nick Clegg walijiuzulu siku ya Ijumaa,pamoja na Kiongozi wa chama cha UKIP Nigel farage kufuatia matokeo mabaya na kuviwacha vyama vyao vikimtafuta kiongozi wa upinzani anayeweza kuuongoza upinzani kuunda serikali mpya.
No comments:
Post a Comment