TANGAZO


Wednesday, April 1, 2015

Uganda kidedea kwenye kriketi

Mpira wa magongo
Michuano ya Afrika ya kriketi ya Daraja la 1 ( T20) inaendelea nchini Afrika ya Kusini huku Uganda ikiendeleza ushindi.
Katika mechi iliyochezwa jana katika uwanja wa Willowmoore Park, uliopi jimbo la Guateng nchini Afrika ya Kusini,
Uganda imeifunga Botswana kwa runs (mikimbio) 58.
Kenya hapo awali iliwafunga Uganda kwa wiketi 8 katika moja ya mechi za mwanzo za ufunguzi na Uganda baadae ilifanya malipizi kwa kuwafunga majirani zao wa Tanzania.
Kenya na Uganda ni miongoni mwa timu zenye nafasi ya kupata nafasi mbili zinazogombaniwa na timu shiriki kwa ajili ya kufuzu kucheza michuano ya kufuzu ya dunia ya ICC Twenty20 itakayofanyika katika nchi za Ireland na Scotland baadae mwaka huu.
wakati huo huo imeelezwa kwamba,nchi za Afrika ya Mashariki zimefungwa katika michuano ya Afrika ya kriketi ya kufuzu Daraja la 1 ( T20) nchini Afrika ya Kusini.
Ghana iliwafunga Uganda kwa runs 5 katika mechi iliyofanyika uwanja wa Sahara Willowmoore Park, moja ya viwanja vya kriketi vikubwa nchini Afrika ya Kusini katika mji wa Benoni, ukiwa na historia ya kuchezwa kwa kombe la Dunia katika miaka ya nyuma.
Mambo yamekwenda kombo kwa Tanzania baada ya kupoteza mechi zote, ambapo kipigo cha mwisho kilitoka kwa Botswana walioshinda kwa runs 35. Tanzania pia ilifungwa na Uganda na Kenya.
Katika mechi za mwisho zilizochezwa Jumanne, Kenya pia ilifungwa na kwa runs (mikimbio) 30. Nigeria waliibuka washindi wa michuano iliyopita huku huku Ghana wakiwa wa pili na Tanzania ikiwa ya tatu.
Ratiba ya leo ya michuano hiyo ni kama ifuatavyo:
Namibia vs. Uganda
Tanzania vs. Kenya
Botswana vs. Ghana

No comments:

Post a Comment