TANGAZO


Friday, April 17, 2015

TRA yawapa somo Wachina kuhusu Sheria za ukusanyaji Kodi nchini

Mkurugenzi wa JITENG Consultant Company Bw. Andrew Huwang akiongea jumuiya ya wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania kuhusu ushiriki wao katika masuala ya ukusanyaji kodi na kuendelea kuongeza ushirikiano kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mwandamizi  Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw.Yeremiah Mbaghi. 
Ofisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Rose Mahendeka akiongea na jumuiya ya wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania kuhusu faida za Mfumo mpya wa Uondoshaji Mizigo (TANCIS) unaosaidia kuongeza ufanisi katika uondoshaji wa Mizigo ya wateja na kuondoa malamiko ya ucheleweshwaji wa huduma hiyo pia kuondoa tatizo la upotevu na mizigo pindi inapoingizwa nchini, wakati wa Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam. 
Ofisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja akiwaeleza wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania kuhusu umuhimu wa kushiriki katika matumizi ya Mashine za Risiti za Kielektroniki (EFD) katika manunuzi na uuzaji wa Bidhaa mbalimbali ili kuiwezesha serikali kupata mapato stahiki bila udanganyifu wakati wa Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam. 
Wanajumuiya wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania wakimsikiliza Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja wakati wa Semina  iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo)

No comments:

Post a Comment