Ofisa Mwandamizi wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Felix Tinkasimile akiwaeleza waandishi wa habari namna mfumo mpya wa uondoshaji mizingo unavyoongeza uwazi na uwajibikaji utakaosaidia kuzuia upoteaji wa mizigo bandarini ikiwemo Magari na Makontena , wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Huduma cha Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Kasty Phelician akiwaeleza waandishi wa Habari majukumu ya kituo hicho ikiwemo kutoa tathnimi ya kodi unayopaswa kulipwa kwa kupitia na kuhakiki nyaraka zote kutoka kwenye kadhia zinazotumia mfumo wa TANCIS ikiwamo viwango vya ushuru wa forodha vinavyopaswa kutozwa.
Meneja wa Forodha Bandari ya Dar es Salaam kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Bw. Burton Kaissy akiwaeleza waandishi wa Habari namna
wanavyoshirikiana na Taasisi mbalimbali kurahisisha usafirishaji wa mizigo yote
inayoenda nje nchi.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Meneja wa Forodha Bandari ya Dar es Salaam kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Bw.Burton Kaissy wakati wa Ziara iliyofanyika katika mamlaka hiyo kuona jinsi mfumo wa TANCIS unavyofanya kazi (Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo)






No comments:
Post a Comment