TANGAZO


Thursday, April 16, 2015

Balozi wa China nchini Tanzania atembelea Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo jijini Dar es Salaam


 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia)  akimweleza  Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (kushoto) namna Wizara yake inavyoendelea kuimarisha shughuli za Mipango Miji, Usimamizi na Matumizi endelevu ya Ardhi katika maeneo mbalimbali nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia),akimweleza Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (kushoto) namna Wizara yake inavyoendelea kuimarisha shughuli za Mipango Miji, Usimamizi na Matumizi endelevu ya Ardhi katika maeneo mbalimbali nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia)  akiwa katika mazungumzo na ugeni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania uliomtembelea leo Ofisini kwake ukiongozwa na Balozi Lu Youqing
(kushoto) kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya China na Tanzania katika kuimarisha  shughuli za Mipango Miji, Usimamizi wa Matumizi endelevu ya Ardhi. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Alphayo Kidata  (kushoto) akifurahia jambo wakati akizungumza na ugeni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania ulioitembelea  Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuendeleza  ushirikiano kati ya China na Tanzania katika  Matumizi endelevu ya Ardhi. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkaribisha  Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing alipomtembelea  ofisini kwake  leo jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo  ya kuimarisha  ushirikiano kati ya Tanzania na China katika masuala ya uendelezaji wa Ardhi na Mipango miji.  

Mkurugenzi wa Mipango  Miji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael Mwalukasa akifafanua jambo kuhusu mipango mbalimbali inayotekelezwa na Tanzania katika kuimarisha matumizi endelevu ya Ardhi wakati wa ziara fupi ya Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing   aliyoifanya katika wizara hiyo leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoonekana ni Kamishna wa Ardhi nchini Dkt. Moses Kusiluka  na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Alphayo Kidata  (kulia). 

Balozi wa China nchini Tanzania Dkt.  Lu Youqing  akitoa ufafanuzi kuhusu uendelezaji wa ushirikiano kati ya China na Tanzania katika katika sekta ya ardhi hususan utoaji wa mafunzo kwa watalaam wa Ardhi, Matumizi endelevu ya Ardhi  na Mipango miji nchini. (Picha zote na Aron Msigwa –MAELEZO)

No comments:

Post a Comment