Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, akimkabidhi Diwani wa Kata ya Msindo, iliyoko Wilaya ya Namtumbo, mkoani Songea, Mohammed Kilowoko, sehemu ya msaada wa tani kumi za saruji zenye thamani ya shilingi milioni mbili na nusu, kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya Msindo iliyoko mkoani humo leo. Wanaoshuhudia (kushoto) ni Meneja wa Fedha Patrick Kyamba na Mkurugenzi wa bodi Margreth Kyarwenda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, akimkabidhi Diwani wa Kata ya Msindo, iliyoko Wilaya ya Namtumbo, mkoani Songea, Mohammed Kilowoko, sehemu ya msaada wa tani kumi za saruji zenye thamani ya shilingi milioni mbili na nusu, kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya Msindo iliyoko mkoani humo leo.

Dar es Salaam, 22 Aprili 2015
KATIKA kuunga mkono jitihada za uboreshaji wa elimu nchini Benki ya Covenant imetoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya Msindo iliyopo Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.
Msaada huo wa vifaa vya ujenzi wa maabara ni mwendelezo wa misaada ambayo imekuwa ikitolewa na benki hiyo katika kuchangia uboreshaji wa elimu katika shule hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Sabetha Mwambenja amesema kuwa lengo la msaada huo ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete wa kuhakikisha kila shule ya Sekondari inakuwa na Maabara pamoja na vifaa vya kutosha.
“Msaada huu una lengo la kuunga jitihada za Mhe. Raisi wa Tanzaia katika kuhakikisha kila shule inakuwa na Maabara na vifaa vyake ili kuongeza tija katika masomo ya sayansi” alisema Mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa.
“Benki yetu imekuwa mdau mkubwa katika maendeleo ya shule hii tangu ilipoanza kujengwa hadi kufikia sasa, nasi tumeitikia wito huo wa kuendelea kuwawezesha” Alisema.
Aidha Mkurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo, Magreth Kyarwenda, amesema kuwa bado benki hiyo itaendelea kuiwezesha shule ya Msindo kufikia malengo yake, Pamoja na kuendelea kuiwezesha jamii ya Watanzania kwa ujumla kwa kuwawezesha kufikia malengo yao.
Kwa Upande wake Diwani wa kata ya Msindo, Mohammed Kilowoko ambae amepokea msaada kwa niaba ya Shule hiyo, ameishukuru benki hiyo huku akitanabaisha kuwa, Elimu katika wilaya ya Namtumbo imekua ya kusuasua, hivyo msaada wa Covenant Bank umekuwa ni mkubwa katika kukomboa elimu wilayani humo kwa namna ambavyo wamekuwa wakijitolea kuwezesha shule hiyo.
“Ninaomba wadau waendelee kujitokeza kutoa msaada katika ujenzi wa shule mbalimbali wilayani namtumbo na kuchangia maendeleo ya elimu wilayani kwetu ili kuinua kiwango cha elimu ambacho kimekuwa chini kwa muda mrefu kwani bado tuna changamoto nyingi zinazotukabili.”

No comments:
Post a Comment