Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akisherehekea na baadhi ya wenyeji wa kijiji cha Nyagisya baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa kijiji hicho.
Waziri wa Maji Prof. Maghembe, akifungua mabomba ya maji ya mradi wa Maji Nyarwana ikiwa ni ishara ya kuzindua miradi hiyo.
Waziri Prof. Maghembe akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili na kuzindua na kuweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa Maji wa Nyarwana kabla ya kuzungumza na wananchi.
Waziri Prof. Maghembe akifungua bomba la maji la mradi wa Maji wa Nyarwana, kuuzindua.
Wanafunzi wa shule ya msingi Nyarwana wakimsikiliza Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyarwana.
Baadhi ya wananchi wa Nyarwana wakimsikiliza Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe (hayupo pichani).
Mwero Kerenge, mzaliwa wa Nyarwanya akimuuliza swali Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe kwenye mkutano wa hadhana baada ya kuzindua na kuweka mawe ya misngi kwenye miradi ya maji.
Claudia Luke mkazi wa kijiji cha Nyaryanya akitoa kero yake kwa Waziri wa Maji, Prof. Maghembe.
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, akizungumza na wananchi wa Nyarwana (hawapo pichani) baada ya kuzindua na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa kijiji hicho.
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe (katikati) akikagua kisima cha Mradi wa Maji Muliba.
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, akiondoka kwenye jengo la mradi wa Muliba, akiwa na wenyeji wake.
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, akifungua bomba la maji la mradi wa Muliba, kuzindua mradi huo.
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, akimtwisha maji mwananchi wa Muliba, baada ya kuzindua mradi wa kijiji hicho.
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Muliba.
Juliana Boke Salima, mkazi wa kijiji cha Muliba, akimuuliza swali Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, katika mkutano uliofanyika kijijini hapo.
Baadhi ya
wananchi wa Muliba, wakimsikiliza Waziri
wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, wakimsikiliza Waziri wa Maji Profesa Jumanne
Maghembe (hayupo pichani) wakati akiwahutubia.
Hussein Makame-MAELEZO, aliyekuwa Tarime
WAZIRI wa
Maji Proefesa Jumanne Maghembe amezitaka kamati za maji za vijiji kuacha
kuifanya miradi ya maji kama biashara badala yake miradi hiyo iwe huduma kwa
wananchi.
Waziri Prof.
Maghembe alitoa tamko hilo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi
kwenye vijiji vya wilaya mbalimbali za mkoa wa Mara baada ya kuzindua na kuweka
mawe ya msingi kwenye miradi ya maji.
Alisema
miradi ya maji inayozinduliwa kwenye vijiji mbalimbali ni huduma lakini baadhi
ya kamati za maji hupandisha bei ya maji kila wiki ili kujikusanyia fedha
nyingi za kutekeleza mambo yao.
Hivyo,
aliwataka wenyeviti wa kamati hizo kuitisha mikutano na wananchi wa maeneo yao ili
kujadili bei ya maji kwa ndoo moja ambayo itakubaliwa na wananchi wote kwa
pamoja na kulipwa na wote.
“Mtakapokuwa
na kamati ya kusimamia mradi wa maji, kamati ijue kwamba mradi wa maji sio
biashara ya maji kwa hiyo hamuwezi kuwa mnapandisha bei ya maji kila siku” alisema
Waziri Prof. Maghembe wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyagasense
wilaya ya Serengeti na kuongeza kuwa:
“Haiwezekani hata kidogo, ni lazima mkae
pamoja na mpange kwamba ndoo moja ya maji mwananchi atachangia shilingi ngapi.
Tukichanga fedha kigodo kidogo kwa ajili ya kuweka kwenye mfuko wetu kila
unapochota maji na kila mnapoknywesha mifugo, nadhani tutakuwa na uwezo wa
kuendesha mradi wetu bila wasiwasi wowote”.
Aliwataka
wananchi hao kuzingatia kwamba kamati ya maji iwe inafanya kazi kwa niaba ya
wananchi na pia iwe inaishirikisha Serikali ya kijiji kwa kila inachofanya na
kwamba wakifanya hivyo watajiendesha vizuri.
Akiwa kwenye
kijiji cha Muriba wilayani Tarime, Waziri wa Maji Prof. Maghembe alisema
wananchi wana haki ya kupata mradi wa maji lakini wanao wajibu kwa kupata haki
hiyo.
Alisema ni
wajibu wa kila mradi wa maji kuwa na kamati ya maji ya kijiji ambayo
itafanyakazi chini ya Serikali ya kijiji na kwamba kila maamuzi wanayoyafanya
kuhusu mradi huo wananchi watatakiwa kuyapitisha.
“Kuwa na
mradi wa maji kuna wajibu, mradi wa maji ni haki yenu tumejenga uko hapa.Na
nyinyi kwa haki hiyo mna wajibu, wajibu wa kwanza ni kuwa na kamati ya kijiji
ya maji. Lakini kamati ile iwe inafanya kazi chini ya uongozi wa Serikali ya
kijiji, sawa hiyo?”alihoji Waziri Prof. Maghembe na kuongeza kuwa:.
“Sasa hii
kamati ikishapanga bei kwamba ndoo moja tutachangia kiasi hiki ili tuweze
kulipa umeme, tulipe walinzi, lazima mapendekezo hayo yaletwe kwenye Serikali
ya kijiji na baadaye yaletwe kwenye mkutano wa kijiji kama huu hapa ili
muyajadili, muyapokee na muyakubali na kuanza kuyafanyia kazi”.
Hivyo
alimtaka mwenyekiti wa kijiji cha Muriba na diwani wa kata hiyo kuhakikisha
kwamba hata wao walipie bei hiyo ya maji bila kujali vyeo vyao ili wapate fedha
za kuendesha mradi huo.
“Mwenyekiti
na wewe mke wako anachota maji, kama ndoo ni shilingi 50 na mke wako alipe 50,
mheshimiwa diwani na wewe mke wako anachota maji, usimpige makofi sasa hivi atarudi
mapema lakini naye alipe shilingi 50” alisema Prof. Maghembe, Waziri wa Maji.
Waziri Prof.
Maghembe alilazimika kutoa muongozo huo kutokana na taarifa kuwepo kwa baadhi
ya kamati za maji za vijiji kutumia miradi hiyo kama biashara ili kutunishia
mifuko ya vijiji kupata fedha za kutekelezea shughuli nyingine za kijiji.
Upatikanaji
wa maji katika vijiji vya mkoa wa Mara unaelezwa kuwa mdogo hata hivyo baadhi
ya vijiji vimefanikiwa kupata maji kwa asilimia 100 baada ya kuzinduliwa kwa
miradi ya maji ya vijiji hivyo.
Uzinduzi wa
miradi ya maji na kuiwekea mawe ya msingi, zilikuwa ni baadhi ya kazi
zilizofanywa na Waziri Prof. Maghembe na baadhi ya viongozi wa mkoa huo ikiwa
ni sehemu ya Maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Maji Kitaifa ambayo ilihitimishwa
Machi 22, mkoani Mara kwa Kaulimbiu isemayo “Maji kwa Maendeleo Endelevu”.
No comments:
Post a Comment