Kaimu Mkuu wa Idara
ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Afisa Bw. Habibu
Msami akimkaribisha Mgeni rasmi kufunga kikao kazi cha kumi cha sekta ya
Utamaduni jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi.
Mgeni rasmi wakati wa kufunga kikao kazi cha
sekta ya utamaduni akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza na wadau wa utamaduni
kuwapongeza kuwa na ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao. Kushoto ni Kaimu
Mkuu wa Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Afisa
Bw. Habibu Msami.
Ofisa Utamaduni
kutoka Kiteto Bibi. Bihawa Masawika akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga kikao
kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni jana Jijini Dar es Salaam.
Ofisa Utamaduni
kutoka Wilaya ya Mbogwe Mkoa wa Geita Bw. Athanas Michael akiimba shairi la
kuhamasisha kudumisha Utamaduni wakati wa kufunga kikao kazi cha kumi cha sekta
ya Utamaduni jana Jijini Dar es Salaam.
Mshairi kutoka Chama
cha Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) Bw. Issa Amiri Kilimo akiimba shairi
la kuipongeza Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana
na wadau wa utamaduni kuhamasisha masuala ya utamaduni wakati wa kufunga kikao
kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni jana Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa
Utamaduni kutoka Wilaya mbalimbali za Tanzania Bara wakifuatilia matukio yaliyokua
yakiendelea wakati wa kufunga kikao kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni jana
Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Genofeva Matemu – Maelezo)
Na Genofeva Matemu –
Maelezo
Tarehe: 07/03/2015
MAOFISA Utamaduni na
wadau wa utamaduni wametakiwa kuuenzi utamaduni wa watanzania kwa kutekeleza na
kusimamia utamaduni ulio sahihi na kuacha kuiga tamaduni zisizokuwa zetu.
Rai hiyo imetolewa jana
jijini Dar es Salaam na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi alipokua akifunga kikao kazi cha kumi
cha Maafisa Utamaduni kutoka Halmashauri zote Tanzania Bara.
Bw. Mushi amesema
kuwa kikao kazi hicho kilichosimamia kauli mbiu isemayo Fani za Sanaa
zielimishe Umma Maudhui ya Katiba pendekezwa kimefanyika wakati muafaka hasa
ukizingatia taifa lipo kwenye hatua ya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga
kura ambalo litatumika pia kupigia kura katiba pendekezwa.
“Sanaa ni shughuli
pana kwa kuwa inaweza kufikisha ujumbe kwa haraka katika jamii hasa kwa kutumia
fani mbalimbali kama muziki, ngojera, ngoma, maigizo na kadhalika hivyo kwa
kupitia fani za Sanaa Umma utaelewa maudhui ya katiba pendekezwa na kufanya
maamuzi sahihi ya kuipigia kura katiba pendekezwa”, alisema Bw. Mushi.
Akizungumza kwa niaba
ya Mkuu wa Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Afisa
Utamaduni Bw. Habibu Msami amesema kuwa kikao kazi cha kumi cha Sekta ya
Utamaduni kimekuwa na mafanikio chanya kwani washiriki wamepata fursa ya kujadili
kwa kina masuala mtambuko yanayoikabili sekta hiyo.
“Ni hakika kuwa
tutakapotoka hapa tutakua mfano mzuri katika Halmashauri na Asasi zetu kwa
kuzingatia mambo ya msingi na kuhakikisha tunautetea, tunaulinda na kuuendeleza
utamaduni wetu kwa ajili ya ujenzi wa Taifa”, alisema Bw. Msami.
No comments:
Post a Comment