TANGAZO


Saturday, March 7, 2015

Watu 10 wafariki katika milipuko Nigeria


Mlipuko Nigeria

Ripoti kutoka Nigeria zinasema kuwa milipuko miwili, imetokea katika mji wa Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno state, kaskazini mashariki mwa nchi.
Mlipuko mmoja umetokea katika soko, ambako inasemekana mshambuliaji wa kujitolea mhanga amewaua watu 10,huku wengine 15 wakijeruhiwa.
Mkuu wa sheria na mahakama katika jimbo la Borno, Kaka Shehu, alisema mashambulio hayo ni ya kikatili na kishenzi.

Mlipuko Nigeria

Mmishonari kutoka Marekani, ambaye alitekwa nyara nchini Nigeria na watu waliojifunika nyuso mwezi uliopita, ameachiliwa huru.
Phyllis Sortor, mwenye umri wa miaka 71, alitekwa kutoka shule ambako alikuwa akifanya kazi, katika jimbo la Kogi, katikati mwa Nigeria, kabla ya kutoroshwa vichakani.
Kanisa lake la Free Methodist, lilithibitisha kuwa mishonari huyo ameachiliwa huru, lakini halikutaka kutoa maelezo zaidi.
Watekaji nyara walitaka kanisa lilipe kikombozi cha dola laki-3, ambayo baadae walipunguza kuwa nusu.
Haijulikani kama kikombozi kililipwa, kabla ya Bi Sortor kuachiliwa huru.

No comments:

Post a Comment