Watazamaji wakifuatilia onesho hilo.
Wakiwa kwenye mafunzo ya muziki.
David twininge akiburudisha.
David twininge akiburudisha.
Emmanuel Muabe.
Emmanuel Muabe.
Wasanii wakitumbuiza.
Wasanii wakitumbuiza.
Wasnii wakitumbuiza.
Wakifundishwa kuogelea.
Wakifundishwa kuogelea.
Mashauri akizungumza na waandishi wa habari.
Mashauri akizungumza na waandishi wa habari.
Pendo Kuzenza akichora.
Pendo Kuzenza akichora.
Wakiwa red carpet kupiga picha.
Wakiwa red carpet kupiga picha.
Wakishangilia kwa shangwe.
Wakishangilia kwa shangwe.
Na Mwandishi wetu, Mwanza
20 Machi 2015
TIGO Tanzania leo imeungana na wanafunzi wa shule ya
kimataifa ya Isamilo pamoja na wasanii kadhaa kutoka Mwanza katika tamasha la
muziki linalokusudia kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wenye
shida mbali mbali kutoka ukanda wa ziwa ikiwemo wanaokumbwa na umasikini na
maradhi.
Harambee hiyo ilihudhuriwa na Meneja Masoko wa
Tigo Kanda ya Ziwa Bw. Ally Mashauri jijini Mwanza ambaye alisema, “Tukio hili
linadhihirisha nia yetu ya dhati ya kuboresha hali ya maisha ya watu nchini
Tanzania. Pesa hii inayochangishwa itawanufaisha mashirika yasiyo ya kiserikali
kama Friends of Children, Saturday School na Forever Angels.
”
“Imekuwa ikirudiwa mara nyingi kwamba elimu ni
ufunguo wa maisha kwa mtu mmoja mmoja, jamii na hata nchi nzima. Ni kwa moyo
huu huu basi Tigo inapenda kuwaunga mkono yatima hawa katika kufanikisha
malengo yao ya kimaisha,” alisema Mashauri.
Mashauri pia alisema kwamba, “Siku
zote tumekuwa tukishiriki katika kutoa mchango wetu kwa jamii, si tu katika
sekta hii ya elimu, bali hata kwa sekta zingine ikiwemo afya, ujasiriliamali
jamii, uwajibikaji kwa jamii na mengine mengi ambayo yamesaidia kuboresha
maisha ya mamilioni ya Watanzania nchini, kama mlivyoshuhudia hivi karibuni
katika kijiji cha Mkwata, Shinyanga ambapo Tigo tulitoa msaada wa kiasi cha
shilingi milioni 30 kwa waathirika wa mafuriko ya mvua.”
“Tunafanya hivi tukiamini ya kwamba
kama kampuni ya Kitanzania, ni wajibu wetu kuendelea kushirikiana na wadau wetu
na serikali katika kujaribu kutoa suluhu kwa changamoto mbali mbali za
kijamiii, ili kuweza kubadilisha maisha ya Watanzania pamoja na uchumi mzima wa
nchi kwa ujumla,” alisema.
No comments:
Post a Comment