TANGAZO


Friday, March 13, 2015

Tanzania kuwa mwenyeji Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na wageni waliofika ofisini kwake kumjulisha kuhusu Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute litakalofanyika nchini Tanzania na kuhusisha nchi 18 tarehe 21 na 22 Machi mwaka huu. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Ramadhani Madabida na anayefuata ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kushoto) akizungumza na waandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute na kuhusisha nchi 18 zikiwemo France, USA, South Africa, Iraq, Mozambique, na Thailand. Kulia ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz na wapili kulia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara. 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Ramadhani Madabida (kulia), akifafanua jambo walipokutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara wakwanza kushoto kumpa taarifa ya Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute litakalofanyika nchini Tanzania tarehe 21 na 22 Machi mwaka huu na kuhusisha nchi 18. katikati ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz. 
Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz (wapili kulia) akielezea jinsi walivyojiandaa kufanikisha Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni litakalohusisha nchi 18 walipokutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (wapili kushoto). Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, na kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Ramadhani Madabida.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na waandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni litakalofanyika nchini Tanzania tarehe 21 na 22 Machi mwaka huu na kuhusisha washiriki kutoka nchi 18 zikiwemo Tunisia, Central Africa, Romania, Nigeria, kongo, Kenya na Uganda. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Utamaduni Bibi. Lily Beleko na kulia ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz. (Picha zote na Genofeva Matemu - Maelezo)

No comments:

Post a Comment