TANGAZO


Sunday, March 22, 2015

SUGU: Sitta ajiandae kwenda The Hague

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbili 'Mr Sugu'

Warioba Igombe,Morogoro
MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbili 'Mr Sugu' amesema kuwa kwa lolote litakalotokea kwenye mchakato wa upigaji kura za maoni na kusababisha uvunjifu wa amani Samwel Sitta lazima ashitakiwe kwenye  Mahakama ya dunia.

Sugu aliyasema hayo mwishoni mwa wiki hii wakati akihutubia mkutano wa hadhara wananchi wa Mkoa wa Morogoro na vitongoji vyake ambapo alisema kuwa Sitta ajiandae kujibu mashtaka  kwa kupindisha maoni ya katiba.

Alisema kuwa wakati wanajiandaa kwenye kinyang’anyilo cha kuchagua Spika wa Bunge la katiba walimpigia debe Sitta wakiamini kuwa ataliendesha bunge kwa misingi ya uaminifu lakini akashindwa kufanya hivyo kwa maslahi ya urais.

“Tulimwamini sana Sitta kukiamini kuwa ataendesha bunge kwa kufuata misingi na kanuni za bunge lakini kwa kuwa alikuwa na taamaa ya urais akaamua kupingisha kanuni kwa kukataa maoni wa wananchi sasa ajiandee kwenda Uhoranzi kujibu mashitaka”alisema Sugu.

Sugu alisema kuwa kitendo cha Sitta kupindisha maoni ya watanzania na kuweka yake kwa matakwa ya kufurahisha chama  chake na kulazimisha kuipitisha katiba mpya kutaweka kuingiza nchi kwenye machafuko makubwa.

Vilevile Sugu aliwataka viongozi wa dini kutojii ngiza kwenye siasa husani kwenye suala zima la katiba na badala lake wawaonye watu kutotenza dhambi ili wapate neema kutoka kwa Mungu.

“Kumekuwa na taarifa za viongozi wetu wa dini kuingilia masuala yasiyowahusu na kusahau kazi yao kubwa ya kungowa watu ili wamkalibie Mungu napenda kutoa rai yangu kwa hawa viongozi kutojiingiza kweye siasa.

Alisema kuwa mfano mzuri ni nchi jirani ya Rwanda viongozi wote wa dini waliojipendekeza kwa Serikali na kushiriki kuuwa watu sasa hivi wanasotea rumande kwa kutumikia vifungo vya mauaji.

Katika mkutano huo uliowahushisha viongozi wa Chama hicho ngazi ya wilaya,mkoa na taifa ulihuthuriwa pia na mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa pamoja na Suzan Kiwanga.
Aliyekuwa Spika wa Bunge Maalum la Katiba, Mbunge wa Urambo Mashariki, ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.

Ambapo Msigwa alisema kuwa taifa letu liko kwenye wakati mgumu kutokana na kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kushindwa kutofautisha Serikali na taifa kitendo kinacho wapa kiburi cha kufanya lolote wanalolisikia.

Msigwa alisema kuwa kuna tofauti kati ya serikali na taifa kwani serkali iliyoko madarakani hata kama ni ya Kidikteta lazima itaondoka madarakani lakini taifa kamwe haliwezi kuondoka.

Alisema kuwa Serikali ya nchi yoyote iko kwa manufaa ya taifa lake laziki serikali ya nchi hii iko kwa manufaa ya chama chake na ndiyo maana Tanzania imeshindwa kuendelea kiuchumi na kubakia kuwa nchi masikini duniani.

“Ndugu zangu wananchi wa Morogoro na watanzania kwa ujumla serikali ya nchi hii imelifanya taifa letu kuwa kama mali yake na kwa kujifanyia mambo yao binafsi pasipo kuandalia manufaa ya watanzania ndiyo maana Tanzania ni kati ya nchi masikini duniani japokuwa tuna lasimali za kutosha”alisema Msigwa.


Aidha alisema kuwa Shirika la Utangazaji la TBC ni redio ya taifa ambapo hata kama CMM wataondoka madarakani bado redio hiyo itaendelea kuwepo lazina kitu cha kusikitisha redio hiyo imekuwa ikitumiwa na CCM kuipigia debe la kura za ndiyo katiba pendekezwa badala ya kutoa elimu kuhusu katiba hiyo.

No comments:

Post a Comment