TANGAZO


Sunday, March 1, 2015

StarTime, Hospitali ya Muhimbili washirikiana kuadhimisha miaka 5 ya Kitengo cha Dharura kwa kuchangia damu

Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Umma wa Star Media Tanzania, Zuhura Hanif (kushoto) akimkabidhi  Kaimu Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa Dharura ya Muhimbili (EMD)  Dk. Hendry Sawe baadhi ya vifaa vitakavyotumika katika zoezi la uchangiaji wa damu salama. Zoezi hilo lilifanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa idara hiyo katika eneo la soko la Karume jijini Dar es Salaam ambapo kampuni hiyo ya matangazo ya luninga kwa njia ya dijitali wakiwa ni moja ya wadhamini.
Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Umma wa Star Media Tanzania, Zuhura Hanif (kushoto) akimkabidhi  Kaimu Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa Dharura ya Muhimbili (EMD)  Dk. Hendry Sawe baadhi ya vifaa vitakavyotumika katika zoezi la uchangiaji wa damu salama. Zoezi hilo lilifanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa idara hiyo katika eneo la soko la Karume jijini Dar es Salaam ambapo kampuni hiyo ya matangazo ya luninga kwa njia ya dijitali wakiwa ni moja ya wadhamini.
Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Umma wa Star Media Tanzania, Zuhura Hanif (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa Dharura ya Muhimbili (EMD)  Dk. Hendry Sawe.
Baadhi ya watu waliojitokeza kuchangia damu salama katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam wakiwa katika banda la kufanyiwa vipimo mbalimbli ikiwemo presha ya damu, uzito na sukari mwilini. Zoezi hilo lilifanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa idara hiyo katika eneo la soko la Karume jijini Dar es Salaam ambapo kampuni ya StarTimes Tanzania wakiwa ni moja ya wadhamini wakuu.
Taswira ya eneo la kuchangia damu salama kwa ajili ya kusaidia Idara ya Wagonjwa wa Dharura ya Muhimbili katika eneo la soko la Karume jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo lilifanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa idara hiyo ambapo kampuni ya StarTimes Tanzania wakiwa ni moja ya wadhamini wakuu.
Msanii wa miondoko ya Hip Hop, akiliwakilisha jiji la Mwanza, Kala Jeremiah (mwenye fulana nyeusi) akiwa tayari kwenda kuchangia damu. 

Taarifa kwa vyombo vya habari
Dar es Salaam, Februari 27, 2015 … 
KATIKA kuadhimisha miaka mitano ya utoaji wa huduma bora za dharura nchini Tanzania licha ya changamoto zinazowakabili kwa wagonjwa kushindwa kulipia, Idara ya Wagonjwa wa Dharura ya Muhimbili (EMD) imeandaa kampeni ya kuchangia damu salama na kutoa elimu ya kuelimisha jamii kuhusiana na uchangiaji damu itakayofanyika katika viwanja vya Karume.

Idara ya Wagonjwa wa Dharura ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni Idara ya kwanza na ya pekee yenye uwezo ikiwa na wataalamu wa huduma kwenye mfumo wa afya ya jamii wa nchini Tanzania.

EMD imeamua kufanya kampeni ya kuchangia damu kwa lengo la kuongeza uwezo wake wa kuwahudumia watanzania ambao wamekumbwa na adha ya ukosefu wa damu kutokana na sababu mbalimbali, moja kubwa ikiwa ni ongezeko la ajali.

Akizungumza wakati wa tukio hilo Kaimu Mkuu wa Idara hiyo Dk. Hendry SAWE alibainisha kuwa, “Idara yetu ni muhimu sana ukizingatia suala la dharura hujitokeza muda wowote bila ya mtu kutarajia. Idara yetu inapokea wagonjwa kati ya 180 na 200 kwa siku, kutokana na ufinyu wa rasilimali kama vile madawa, vifaa na damu salama ya kuwahudumia wagonjwa hawa tumeona ni vema katika maadhimisho ya siku hii basi tukafanya kitu ambacho kitasaidia katika kuijengea idara yetu uwezo.”

“Siku ya leo tunaadhimisha miaka mitano ya Idara yetu, tukijivunia kabisa kwa kuwa na huduma bora na wataalamu. Leo tumekusanyika hapa sio tu kushereheka safari hiyo ndefu tuliyoianza miaka michache iliyopita bali pia kutathimini umuhimu wa idara hii na kuweza kuijengea uwezo ili ijiendeshe yenyewe na kuweza kuwahudumia maelfu ya watanzania ipasavyo. 

Hivyo basi leo tutaelimishana juu ya masuala mbalimbali ya afya na pia kuchangia damu itayowawezesha wagonjwa wanaokuja kwenye idara yetu kupatiwa huduma, usishangae inaweza ikatokea ukawa wewe, mtoto wako, ndugu yako au mzazi wako.” Aliongezea Dk. Sawe

Kaimu Mkuu wa Idara hiyo katika kutambua mchango wa wahisani waliojitokeza katika shughuli hiyo aliipongeza kampuni ya Star Media Tanzania ambao ni wasambazaji na wauzaji wa ving’amuzi vya StarTimes nchini kwa moyo wao wa kujitolea na kuunga mkono tukio hilo licha ya muda mfupi tangu kupata taarifa za tukio hilo.
“Ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru wahisani na wafadhili mbalimbali waliojitokeza na kutuunga mkono kwa kujumuika nasi siku hii ya leo. Nawapongeza sana StarTimes kwa ushiriki wao na kutufadhili vifaa na madawa pamoja na mahema ambavyo vimekuwa na umuhimu mkubwa katika kufanikisha zoezi hili. 
Hatuna cha kuwalipa ila kikubwa tunachoweza kusema kwamba msaada wenu umekuwa wa thamani kubwa kwetu na nina matumaini tutaendelea kushirikiana kadiri siku zinavyokwenda, asanteni sana.” Alimalizia Dk. Sawe

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Umma wa StarTimes Tanzania, Bi Zuhura Hanif alisema kuwa wao wamefarijika sana kwa idara hiyo ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwafikiria kama wadhamini na kuwafuata kutaka msaada.
“Kusema ukweli inatia faraja sana na fahari kwetu sisi kwa taasisi kubwa ya kitaifa kama Muhimbili kwa kuweza kutambua uwepo wetu na kama moja ya wadhamini. Hii ni ishara nzuri kwamba uwepo wetu katika jamii ya watanzania ni mkubwa, unatambulika na kuthaminika. 
Nasi tulifurahi sana tulipoletewa taarifa za tukio hili ingawa ilikuwa ndani ya muda mfupi lakini tumeona kwa uwezo wetu kutoa msaada wa vifaa, madawa, vinywaji na vitafunwa pamoja na mahema ili kusaidia kufanikisha zoezi hili zima kwani ni kwa manufaa ya watanzania wote ambao asilimia kubwa ni wateja wetu.” Alisema Bi Hanif

Mkurugenzi huyo alimalizia kwa kusema kuwa, “Natoa wito kwa taasisi na makampuni mengine kujitokeza na kuunga mkono jitihada kama hizi ambazo zinalenga kuwapatia watanzania huduma bora za afya. 
Katika matukio kama haya ningewaomba tuwe tunaona kama tunawasaidia kuwapatia wateja wetu afya nzuri. 

Na pia ningependa kuipongeza idara hii kwa jitihada hii waliyoifanya kwani wakati mwingine sio kila kitu kuitegemea serikali kuu katika kuwezesha kila kitu, wapo wadau, wahisani na wafadhili ambao wanaweza kuwezesha shughuli kama hizi cha msingi ni namna na njia nzuri ya kuwafuata na kuwashawishi.”

“Na mwisho kabisa ningependa kuchukua fursa hii kuwapongeza wale wote waliojitokeza katika kuchangia damu na kupata elimu nzuri ya afya, kwani kujitolea kwao leo kumeokoa maisha ya watanzania wengi kwa namna moja ama nyingine.” Alihitimisha Bi Hanif.
Katika kufanikisha zoezi hilo StarTimes Tanzania walitoa msaada wa vifaa kama vile mashine tatu za kupimia presha ya damu (BP Machines), mashine sita za kupimia sukari (RBG Machines) na mashine moja ya kupimia uzito (Weighing Machine) pamoja na vinywaji kwa ajili ya wale waliojitokeza kuchangia damu.

No comments:

Post a Comment